Home KITAIFA RAIS DK SAMIA AZINDUA HOSPITALI KUBWA YA RUFAA KANDA YA KUSINI

RAIS DK SAMIA AZINDUA HOSPITALI KUBWA YA RUFAA KANDA YA KUSINI

Google search engine

Na MWANDISHI WETU

-MTWARA

Rais wa Dk. Samia Suluhu Hassan, amezindua Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini iliyopo katika eneo la Mitengo Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara.

Uzinduzi huo umefanyika leo Septemba 15,2023 akiwa katika ziara yake ya kikazi ya siku nne yenye lengo la kukagua  utekelezaji wa miradi ya maendeleo  na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya  Chama Cha Mapinduzi  ya mwaka 2020-2025.

Akizungumza katika hafla hiyo ya uzinduzi, Rais Dk, Samia amewaasa wahudumu na watumishi wa hospital hiyo kutunza majengo pamoja na vifaa tiba pamoja na kuwakumbusha matumizi ya lugha sahihi wanapotoa huduma kwa wananchi n wagonjwa wanapofika hospitalini hapo.

Pamoja na uzinduzi wa majengo na vifaa tiba katika hospitali hiyo, Mkuu huyo wa nchi amekabidhi funguo za magari ambayo yanatoa huduma ya Mkoba, ambayo ni mahsusi kwa ajili ya kubebea na kutoa huduma kwa wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU), ambapo mgonjwa kutoka hospitali za pembezoni na Hospital ya Rufaa ya Kanda ya Kusini atapatiwa huduma akiwa njiani huku akiwahishwa hospitali kwa matibabu zaidi.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here