Na MWANDISHI WETU
-BEST MEDIA, DAR ES SALAAM
Mabingwa wa Ligi kuu Tanzania Bara, Yanga SC, wameendelea kuonyesha ubabe wao katika uga wa kimataifa kwa kufanikiwa kuichabanga timu ya Al-Merrikh mabao 2-0 katika mchezo ambao umepepetwa kwenye dimba la Pele Jijini Kigali nchini Rwanda.
Katika mchezo huo Yanga SC, ilitoka kifua mbele kwa kuifunga mabao hayo kupitia kwa washambuliaji wao Kenned Musonda pamoja na Clement Mzize ambapo mabao hayo ya ushindi yalipatikana kipindi cha pili cha mchezo.
Hata hivyo kwa upande wa Wekendu wa Msimbazi, Simba SC ilishindwa kutamba katika Uwanja wa Ndola nchini Zambia baada ya kulazimisha sare ya mabao 2-2 ambayo yalifungwa na ‘Mwamba wa Lusaka’ Claotos Chama.
Pamoja na Simba kuumiliki mchezo huo ulipigwa kwa dakika 96, ilishindwa kuonyesha makali kali ya kufunga mabao licha ya kupata nafasi kadhaa katika mchezo huo.