Na. Andrew Chale
-Zanzibar
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar [SMZ] kupitia kwa Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na michezo, Tabia Maulid Mwita, ameishukuru kampuni ya simu ya Halotel kwa kusaidia vifaa vya usafi katika shamrashara za sku ya usafi duniani, iliyofanyika mapema leo Septemba 16, katika fukwe ya Maruhubi Visiwani Zanzibar.
‘’Changamoto inayotukabiri ni suala la vifaa vya kuhifadhia usafi, tunaweza kufanya usafi lakini sehemu ya kuhifadhia hakuna.
Tunao wananchi wa kutunza usafi, lakini vifaa vya kuhifadhia takataka hakuna, ni tatizo kubwa kwa hivyo niombe wadau kusaidia suala hili.
Naagiza wadau na watendaji wengine wa serikali kuhakikisha mnashirikiana nao katika kuboresha mazingira yetu’’. Amesema Waziri Tabia Mwita.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halotel Zanzibar, Abubakar Adamu Ngatomela amesema kuwa, Wameamua kuiunga mkono serikali ya SMZ katika kufanya usafi hasa maeneo ya sekta ya Utalii ikiwemo fukwe, ambazo watalii wengi ufika kwani utalii unamchango mkubwa katika uchumi wa Zanzibar.
‘’Halotel ambao tunapatikana katika maeneo ya Unguja na Pemba kwa Zanzibar tunawafikia wananchi mbalimbali hivyo vifaa hivi vitaleta chachu kubwa katika kutunza mazingira yetu, sambamba na kampeni yetu ya Ishi nao’ amesema Abubakar .
Nae Mkurugenzi Idara ya Utalii katika Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale, Dkt. Abdallah Mohmed amesema, wameanza kushirikiana na wadau mbalimbali katika upatikanaji wa vifaa vya usafi kama walivyofanya kampuni ya Halotel walioshiriki kutoa vifaa vya usafi.
Vifaa vilivyotolewa na kampuni ya Halotel ni pamoja na Mafyagio, gloves, Madebe ya uhifadhia taka yenye magurudumu, barakoa, bips, reki na vingine vingi.
Katibu Mkuu Wizara ya Utalii na Mambo ya kale, Fatma Mabrouk Khamis amesema zoezi hilo kwa sasa litakuwa endelevu kwa kufanyika kila mwezi.
Zoezi hilo ambalo limeandaliwa na Wizara hiyo ya Utalii na Mambo ya Kale, wadau mbalimbali wameshirikiana kama KVZ, Vikundi vya mazoezi Jumuiya ya mazoeiz Zanzibar, Fisherman Tour, na wengie wengi.