Home KITAIFA DC KASILDA AONGOZA MJADALA WA MAPATO KWA TAASISI

DC KASILDA AONGOZA MJADALA WA MAPATO KWA TAASISI

Google search engine
Mkuu wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni akiongoza kikao ca kujadili hali ya mapato kwa taasisi za Serikali wilayani hapa

Na MWANDISHI WETU

-SAME

MKUU wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni ameongoza wajumbe wa Kamati ya Usalama wa wilaya hiyo, kwenye kikao cha kujadili mapato ya taasisi mbalimbali za Serikali huku akiagiza kikao hicho kufanya kila mwezi ili kuona tija ya hali ya mapato kwa taasisi za serikali.

Hayo ameyasema leo Septemba 23, 2023, ambapo amesema kuwa lengo la kuagiza kikoa hicho kufanyika kila mwezi ni njia sahihi ya kuhakikisha ufuatiliaji unapokuwpo kwa taasisi husika.

“Pamoja na ufuatiliaji pia kama njia ya kuhakikisha taasisi zote zinafikia malengo kwenye kukusanya mapato sambamba na kutafuta ufumbuzi wa haraka pindi changamoto zinapobainika kwa kujua na kufuatilia hali ya mwenendo wa makusanyo kwa kila mwezi,” amesema Mgeni

Katika kicho ambacho kimejadili mapato ni pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Same, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Hifadhi ya Taifa Mkomazi, Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyama Pori Tanzania (TAWA),  Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA).

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here