-BODI YA REA YAVUNJWA, JOHN ULANGA ARUDISHWA TTCL
Na MWANDISHI WETU
-BEST MEDIA, DAR ES SALAAM
RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameendelea kufanya mabadiliko ndani ya Serikali yake huku aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Maharage Chande, akuhamishwa tena na kupelekwa kuwa Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania akichukua nafasi ya Macrice Mbodo, ambaye atapangiwa kazi nyingine,
Taarifa iliyoletwa leo Septemba 25, 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Zuhura Yunus, imekuja ikiwa izpita siku tatu tangu kufanyika kwa mabadiliko ya awali ambapo Maharage, aliyehamishiwa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) akitokea kuongoza Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).
Maharage Chande, ambaye alichukua nafasi ya Peter Ulanga, ambaye katika taarifa ya Ikulu ya leo Sepetmba 25, 2023, amerudishwa tana kuendelea na wadhifa aliokuwa nao awali wa kuliongoza Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).
Pia katika uteuzi huo pia Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Mkurugenzi wa Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) John Ulanga, kuwa Balozi ambapo taapishwa leo na viongozi wengine wateule walioteuliwa Septemba 23, 2023.
Panga hilo la Rais Samia pia limetua ndani ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), ambapo amevunja bodi yaw akala hiyo, iliyokuwa ikiongozwa na Janeth Mbene na kumteua Jenerali Mstaafu Jacob Kingu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi.