Home KITAIFA MSD YAELEZA UPATIKAJI DAWA, VIFAA TIBA ULIVYOIMARIKA NCHINI

MSD YAELEZA UPATIKAJI DAWA, VIFAA TIBA ULIVYOIMARIKA NCHINI

Google search engine

-SASA YAJIPANGA KUWEKEZA KWENYE VIWANDA VYA NDANI, KUWA TEGEMEA KWA NCHI ZA SADC

Mkurugenzi Mkuu wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD), Mavere Tukai, akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari leo Septemba 27,2023 katika mkutano wa ulioratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD), Mavere Tukai (kushoto), akiwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Msajili wa Hazina, Erick Mkuti, leo Septemba 27, 2023, Jijini Dar es Salaam
Baadhi ya Wahariri walioshiriki mkutano huo leo Septemba 27, 2023, Jijini Dar es Salaam
Meneja Uhusiano wa MSD, Etty Kusiluka, akizungumza katika mkutano huo leo Sepetmba 27, 2023 Jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Msajili wa Hazina, Erick Mkuti, akiteta jambo na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile, leo Septemba 27, 2023

Na MWANDISHI WETU

-BEST MEDIA, DAR ES SALAAM

MKURUGENZI Mkuu wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD), Mavere Tukai, ameeleza mafanikio ya kadhaa ya taasisi hiyo, ikiwamo kuimarika kwa huduma ya dawa, vifaa tiba na vitendanishi katika hospitali nchini.

Kutokana na hali hiyo amesema kuwa moja ya mkakati ambao sasa wanakwenda kuutekeleza ni kuhakikisha wanasimamia mkakati wao wa kuanzisha viwanda vya ndani na kwa lengo la kuwalinda wazalishaji wa nchini.

Akizungumza leo Septemba 27, 2023 Jijini Dar es Salaam katika mkutano ulioratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina na Wahariri wa Vyombo vya Habari, ambapo amesema kuwa MSD imeendelea kufanya maboresho ya kiutendaji kama ilivyoelekezwa na Rais Samia Suluhu Hassan, huku mabadiliko hayo yakilenga kuimarisha upatikanaji wa bidhaa za afya pamoja na utawala bora.

Amesema serikali ya awamu ya sita kwa mwaka wa Fedha 2022/23, ilitenga Sh bilioni 200 za ununuzi wa bidhaa za afya nchini ikiwamo pia kuimarisha upatikanaji wa bidhaa za afya nchini.

Mavere amesema MSD inaendelea na usambazaji wa bidhaa za afya kwenye vituo vyote vya afya vya Serikali takribani 7,153 kupitia kanda zake 10 zilizowekwa kimkakati, ambapo kwa sasa usambazaji huo unafanyika mara sita kwa mwaka, kutoka mara nne za awali.

ONGEZEKO LA FEDHA KWA UNUNUZI WA BIDHAA ZA AFYA

Tukai, amesema kuwa fedha iliyopokelewa mwaka wa fedha 2022/23 ni Sh bilioni 190.3 ikilinganishwa na Sh bilioni 134.9 mwaka wa fedha 2021/22, sawa na asilimia 95.

HALI YA MAPATO MWEZI AGOSTI 2023

“Mapato kwa mwezi Agosti 2023 lengo ni Shilingi bilioni 35.68, utendaji halisi Shilingi bilioni 34.08,” amesema

Kutokana na hali hiyo, amesema kuwa kwa sasa MSD inajitegemea katika uendeshaji wake licha ya Serikali kuendelea kuwapa fedha kwa ajili ya ununuzi wa dawa, vifaa tib ana vitendanishi, jambo ambalo aliishukuru Serikali ya Rais Dk. Samia, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu pamoja na Wizara ta Fedha ambayo hivi karibuni ilitangaza kuwaongezea mtaji wa fedha.

UNUNUZI WA BIDHAA ZA AFYA

Kuanzisha Kitengo Maalumu cha Usimamizi na Ufuatiliaji wa Mikataba

Ununuzi wa bidhaa za afya kutoka kwa wazalishaji wa ndani umeongezeka kutoka shil bil 14.1 mwaka wa fedha 2021/22 hadi kufikia Sh bilioni 39.77

Kutoagiza bidhaa kutoka nje ya nchi zile ambazo zinakidhi mahitaji na viwango vya ubora hivyo kutegemea wazalishaji wa ndani

Kuanzisha zabuni maalumu zinazohusu wazalishaji wa ndani hivyo kuongezea uwezo wa uzalishaji.

Kuongeza idadi ya mikataba ya muda mrefu kutoka mikataba 100 yenye bidhaa za afya 711 kwa mwaka wa fedha 2021/22 hadi kufikia mikataba 233 yenye bidhaa 2,209 kwa mwaka wa fedha 2022/23.

USAMBAZAJI WA BIDHAA ZA AFYA

Amesema kuimarisha mfumo wa usambazaji kwa kusambaza bidhaa za afya mara sita kwa mwaka (kila baada ya miezi miwili) kwa mwaka wa fedha 2022/23 badala ya mara nne  kwa mwaka (miezi mitatu) hivyo kupunguza muda wa vituo vya afya kusubiri bidhaa za afya.

“Kununua matrela 16 yenye thamani ya Shilingi bilioni 2.6 ili kuongeza kasi ya usambazaji wa bidhaa za afya, kuongeza usambazaji wa bidhaa za afya kwa asilimia 16 kutoka Shilingi bilioni 320 kwa mwaka wa fedha 2021/22 hadi shilingi bilioni 373 kwa mwaka wa Fedha 2022/23,” amesema

UZALISHAJI WA BIDHAA ZA AFYA

Amesema wataendelea kuimarisha uzalishaji wa bidhaa ikiwamo kiwanda cha bidhaa za mikono “gloves” kilichopo Idofi, mkoani Njombe.

“Kuhusisha sekta binafsi kwa kutambua maeneo ya uwekezaji ya bidhaa za afya za kimkakati za vidonge (tablets), rangi mbili (capsules), vimiminika, na bidhaa zitokanazo na zao la pamba na kutangaza matamanio ya ushirikiano kati ya MSD na sekta binafsi

“Kukamilisha taratibu za usajili na uendeshaji za kiwanda cha barakoa cha N95 kilichopo Keko ambapo uzalishaji wake utakidhi mahitaji ya barakoa nchini. Kuboresha mifumo simamizi kwa kutumia TEHAMA mfano; mfumo wa usimamizi wa magari pamoja na kuanzisha Kampuni tanzu ili kuweza kusimamia shughuli za uzalishaji wa bidhaa za afya kwa ufanisi

ugatuzi wa utendaji kutoka makao makuu kwenda Ofisi za Kanda,” amesema

MIRADI

“Aidha kwa upande wa uzalishaji wa bidhaa za afya MSD imeendelea na uzalishaji barakoa, huku mradi wa wa viwanda vya Idofi ulioko Makambako uko hatua za mwisho, ambapo ukikamilika utazalisha mipira ya mikono (Surgical & Examination Gloves), vidonge (tablets), rangi mbili (capsules), vimiminika (syrup), na dawa za ngozi (ointment & cream).

“Miradi hii chini ya MSD itasaidia kuimarisha upatikanaji wa bidhaa za afya nchini. Katika hatua nyingine ameongeza kuwa MSD imeendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi, ili kushiriki katika ujenzi wa viwanda nchini kwa njia ya ubia kati ya Serikali na Sekta Binafsi (PPP), ambapo hadi sasa mchakato huo unaenda vizuri,” amesema

Mavere, amesema kuwa utekelezaji wa majukumu ya MSD unaenda sambamba na utekelezaji wa maelekezo ya maboresho ya utendaji yaliyotolewa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, wakati alipoteua uongozi mpya wa Bohari hiyo.

Amesema kuwa MSD inapitia mifumo yote ya uendeshaji ikiwemo mnyororo wa ugavi, usimamizi na TEHAMA ili kuendana na kasi ya ongezeko la ujenzi wa vituo vya kutolea huduma za afya, vinavyojengwa na Serikali na kuhakikisha malengo ya Serikali katika upatikanaji wa bidhaa za afya yanafikiwa.

“Pia tuna kampuni tanzu ambapo pia kwa sasa mkakati wetu ni kuanza uzalishaji katika Kiwanda chetu cha Keko,” amesema Mkurugenzi Mavere

UFANISI KWA NCHI ZA SADC

Mavere, amesema kuwa kuwa kinara kwa usambambazaji wa dawa kwa nchi za Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kwa kuwa Bohari ya Dawa Tanzania (MSD) imekuwa mfano wa kuigwa katika nchi za jumuiya hiyo.

Amesema MSD imekuwa chachu ya kuunganisha maendeleo na kukuza uchumi wa Afrika kutokana na ufanisi wake katika  upatikanaji wa uhakika wa dawa na bidhaa za afya.

Tukai amesema kuwa jumuiya ya SADC imelenga imetoa kibali kw ana kuifanya taasisi hiyo kuwa msambazaji wa dawa kwa nchi husika.

Amesema hatua ya uanzishaji wa Kampuni Tanzu “MSD Medipharma Manufacturing Company Ltd” ambayo itakayosimamia uzalishaji wa bidhaa za afya ni moja ya mafanikio ambayo wamekuwa wakijivunia katika utendaji wao

“Nchi ambazo zimewahi kutumia mpango wa ununuzi wa pamoja Tanzania, Comoro, Seychelles ambapo thamani ya bidhaa ambazo zimewahi kuuzwa kupitia mpango huu ni Shilingi bilioni 6.8.

“Hata hivyo hadi sasa mahitaji ya nchi zifuatazo yapo katika ukamilishaji ambazo ni Zambia, Malawi,” amesema Tukai

Akizungumzia changamoto katika ushiriki wa Ununuzi wa pamoja ni wa hiari, ikiwamo hatua zinazochukuliwa ili kuongeza ufanisi kama njia ya kuboresha ushirikiano na kuongeza ushawishi katika ngazi ya SADC Sekretarieti na katika ngazi ya nchi za SADC kupitia balozi zetu.

Mbali na hilo Mkurugenzi huyo wa MSD, amesema kuwa hatua ya kushirikisha viwanda vilivyopo nchi za SADC kwenye mpango wa ununuzi wa pamoja kama njia ya kuimarisha hatua hiyo muhimu kwa nchi wanachama.

CHANGAMOTO

Akizungumzia ushiriki wa ununuzi wa pamoja Tukai, amesema  ni wa hiari huku lengo kubwa likiwa ni kuimarisha mifumo ya usimamizi kwenye ununuzi na usambazaji wa bidhaa za afya

“Kuimarisha ushirikiano na wadau wa mnyororo wa ugavi,  kushirikisha balozi zetu zilizopo China, Algeria, Urusi na Korea ya Kusini kutafuta wadau wa uzalishaji na ununuzi na kutumia wadau wa ndani na nje ya nchi ili kuongeza uzalishaji wa bidhaa za afya nchini,” amesema

USAMBAZAJI

“Usambazaji ni moja kwa moja kwenye vituo, usambazaji unafanyika kila baada ya miezi miwili na makabidhiano yanafanyika kwa mfumo (PoD) pamoja na kuhakikisha upatikanaji wa bidhaa za afya kwa uhakika katika vituo vya kutolea huduma za afya,” amesema

UFANISI WA BOHARI YA DAWA

Tukai amesema kuwa MSD ina magari 185 ya usambazaji na watumishi zaidi ya 688 pamoja na kusimamia kampuni tanzu.“Kanda 10 za MSD ambazo nazo zinafanya kubwa ya kurahisisha huduma za upatikaji wa dawa, vifaa tib ana vitendanishi ambazo ni Dar es Salaam, Tanga, Kilimanjaro, Iringa, Mbeya, Mwanza, Tabora, Kagera, Mtwara na Dodoma” amesema Tukai

Amesema kwa sasa wana viwanda vya kuzalisha bidhaa za afya viwili pamoja na kuhudumia vituo zaidi 7,600 vya afya pamoja na hospitali.

MAFANIKIO

Akizungumza mafanikio ya MSD, Mkurugenzi huyo  amesema kuwa kuimarika kwa upatikanaji wa bidhaa za afya ambao umeongezeka kutoka asilimia 51 mwezi Juni 2022 hadi kufikia asilimia 64 Juni 2023

“Upatikanaji wa Dawa umefikia asilimia 81 mwezi Juni 2023 kutoka asilimia 57 mwezi Juni 2022,” amesema

Mwisho

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here