Home KITAIFA DC KASILDA AONYA WACHIMBA MADINI WALIOVAMIA VYANZO VYA MAJI

DC KASILDA AONYA WACHIMBA MADINI WALIOVAMIA VYANZO VYA MAJI

Google search engine
Mkuu wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni, akiongoza wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama kwenye ukaguzi wa machimbo ambayo yapo jirani na vyanzo vya maji
Baadhi ya mashimo ya wachimbaji wa dhahabu yalipo jirani na vyanzo vya maji
Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni akitoa maelekezo katika eneo ambalo linadaiwa kuwa na wachimbaji wa dhahabu ambao wanaharibu vyanzo vya maji
Vyanzo vya maji vilivyopo katika eneo ambalo linadaiwa kuvamiwa na wachimbaji wa dhahabu

Na ASHRACK MIRAJI

-SAME

MKUU wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni ametahadharisha tabia ya uwepo wa baadhi ya watu wanaoingia kinyemela na kuanza kuchimba madini katika maeno ambayo ni yapo chanzo cha maji.

 Chanzo hicho cha maji kinacho tegemewa na zaidi ya wakazi 21,000 wa Kata za Kisiwani na Msindo wilayani hapa, ambapo watu hao wanavunja sheria na watachukulia hatua na Serikali.

Onyo hilo alilitoa juzi wakati Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ilipofanya oparesheni maalumu ya kushtukiza baada ya kupokea taarifa za kuwepo shughuli za uchimbaji madini ya dhahabu unaofanyika kinyume na taratibu za kisheria.

DC Kasilda amesema kuwa taarifa zilizomfikia ni kwamba mbali na wachimbaji hao kufanya shughuli zao kinyemela pia wanatumia vyanzo vya maji ambavyo vipo karibu na machimbo hayo kusafishia madini wakitumia pia Mercury na kuhatarisha usalama wa watumiaji wengine wa maji hayo.

“Kuingia huku kinyemela na kuharibu miundombinu ya maji ni hujuma hatutavumilia vitendo kama hivi, niwatake Jeshi la Polisi kuweka kambi kwenye eneo hili kuimarisha ulinzi kuhakikisha shughuli za uchimbaji zinakoma na waliohusika kuihujumu Serikali lazima watafutwe popote na wachukuliwe hatua,” amesema DC Kasilda

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here