Home KITAIFA Benki ya NMB yaendelea kutoa elimu ya kifedha kwa wafanyabiashara Jijini Dar...

Benki ya NMB yaendelea kutoa elimu ya kifedha kwa wafanyabiashara Jijini Dar es Salaam

Google search engine
Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, Karolina Mthapula (kulia) akipokea tisheti kutoka kwa Meneja wa Benki ya NMB kanda ya kaskazini, Ladislaus Baraka (kushoto). Tisheti zitakazovaliwa na katika maadhimisho ya Kilele cha mbio za mwenge nchini ni miongoni mwa udhamini wa shilingi milioni 62 wa Benki ya NMB katika kufanikisha shuguli hiyo pamoja na maonesho ya wiki ya Vijana kitaifa, shuguli ambazo zote zinafanyika Babati, Mkoani Manyara.

Na MWANDISHI WETU

Benki ya NMB kupitia Klabu za Biashara yaani ‘NMB Business Club’ jana iliandaa mafunzo ya kifedha kwa wafanyabiashara Jijini Dar es Salaam ikiwa ni utekelzaji wa mkakati wa benki hiyo wa kuongeza ushirikishwaji wa kifedha.

NMB Business Club ni jukwaa la benki ya NMB linalolenga wateja wadogo na wa kati (MSME) na linawapa wafanyabiashara fursa ya kukutana na kubadilishana mawazo ya biashara, mbinu bora za soko na huwawezesha kupata mafunzo kuhusu mada mbalimbali za biashara.

Mafunzo hayo yalijumuisha moduli mbalimbali za biashara ikiwa ni pamoja na ufadhili endelevu, uchambuzi wa gharama, uandaji wa bajeti na utunzaji wa kumbukumbu.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku moja yaliyowakutanisha mamia ya wafanyabiashara Jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Dismas Prosper alisema benki yake imejipanga kuendelea kutoa elimu ya kifedha kwa wateja wake ili kuwawezesha kufanya maamuzi sahihi.

“Elimu ya kifedha ni kipaumbele kwa Benki ya NMB. Tayari tumetoa mafunzo mbalimbali ya kifedha kote nchini mwaka huu kama sehemu ya utekelezaji wa dhamira yetu ya kuimarisha ujumuishaji wa kifedha. Elimu ya kifedha imekuwa jambo la lazima kwa kila mtu hasa kwa wafanyabiashara ndiyo maana tunajitahidi kila mara kama benki kuiboresha,” alisema.

Prosper alisema kuwa benki yake ya NMB itaendelea kutumia wataalam kutoa elimu ya masuala ya kifedha ili kuwawezesha wateja wake kufanya vizuri huku akibainisha kuwa benki yake vilevile hutumia fursa hiyo kusikia changamoto zinazowakabili wafanyabiashara.

“Majukwaa ya mafunzo ya Klabu za Biashara ya NMB sio tu kwamba yanatoa ujuzi wa kifedha lakini hutuwezesha kupata maoni ya wateja na kuongeza uhusiano na wateja wetu wa biashara,” aliongeza.

Prosper wakati wa hafla hiyo alisisitiza dhamira ya benki hiyo ya kuendelea kutoa suluhu za kibenki kwa wateja wake na kuwataka wafanyabiashara kuchangamkia suluhu za malipo za kidijitali za benki hiyo,”

Kwa upande wake Mwenyekiti wa NMB Business Club Kanda ya Dar es Slaam Award pandilah wakati wa hafla hiyo aliipongeza benki hiyo kwa kujitolea kusaidia ukuaji wa wafanyabiashara kote nchini huku akisema kuwa benki hiyo imekuwa chachu ya biashara nyingi nchini.

Hata hivyo aliitaka benki hiyo kuzingatia kupunguza riba za mikopo ili kuwawezesha wafanyabiashara wengi  kuchukua mikopo yakuendeleza biashara zao.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here