Home KITAIFA BUNGE LA TANZANIA NA SHIRIKA LA UNDP WASAINI MKATABA WA DOLA MILION...

BUNGE LA TANZANIA NA SHIRIKA LA UNDP WASAINI MKATABA WA DOLA MILION 2.5

Google search engine
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa UNDP, Sergio Valdini wakisaini andiko la Mradi wa awamu ya tatu la kuwajengea uwezo Wabunge na Watumishi wa Bunge lenye thamani ya Dola za Kimarekani 2,596,001.00 katika Ofisi Ndogo za Bunge zilizopo Jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Katibu wa Bunge, Nenelwa Mwihambi akishuhudia tukio
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Sergio Valdini katika Ofisi ndogo za Bunge zilizopo Jijini Dar es Salaam leo tarehe 11 Oktoba, 2023
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson akibadilishana hati na Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa UNDP, Sergio Valdini mara baaada ya kusaini andiko la Mradi wa awamu ya tatu la kuwajengea uwezo Wabunge na Watumishi wa Bunge

Bunge la Tanzania na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) wamesaini andiko la Mradi wa Awamu ya Tatu wa Kuwajengea uwezo Waheshimwa Wabunge na Watumishi wa Bunge (LSP III) wenye thamani ya Dola za Kimarekani 2,596,001.00. Aidha, Mradi huo utahudumia pia Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

Andiko hilo limesainiwa leo tarehe 11 Oktoba, 2023 katika Ofisi Ndogo za Bunge zilizopo Jijini Dar es Salaam ambapo Utekelezaji wa Mradi huo utaanza Mwezi Oktoba 2023 hadi Novemba 2027.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here