Home KITAIFA KAMPUNI YA AIRPLANES AFRICA LIMITED YAZINDUA NDEGE YA KWANZA KUTENGENEZWA TANZANIA

KAMPUNI YA AIRPLANES AFRICA LIMITED YAZINDUA NDEGE YA KWANZA KUTENGENEZWA TANZANIA

Google search engine
Ndege ya kwanza kutengenezwa Tanzania nchini ikiwa kwenye maonyesho ya kimataifa ya wazalishaji wa bidhaa za Viwandani Tanzania yajulikanayo kwa jina la Tanzania International Manufacturers Expo 2023 (TIMEXPO) yaliyomalizika hivi karibuni  kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam. Ndege hiyo Na.1 imetengenezwa na wataalamu wazawa kwa kushirikiana na wenzao kutoka Jamhuri ya Czech wa kampuni ya Airplanes Africa Limited (AAL)  ya mkoani Morogoro.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila akizindua ndege ya kwanza kutengenezwa nchini na kampuni ni ya Airplanes Africa Limited (AAL) yenye makao yake makuu mkoani Morogoro. Uzinduzi huo ulifanyika wakati wa maonyesho ya kimataifa ya wazalishaji wa bidhaa za Viwandani Tanzania yajulikanayo kwa jina la Tanzania International Manufacturers Expo 2023 (TIMEXPO) yaliyomalizika hivi karibuni  kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam

Na MWANDISHI WETU

-DAR ES SALAAM

NDEGE ya kwanza kutengenezwa Tanzania imetambulishwa rasmi na kampuni ya Airplanes Africa Limited (AAL) ya mkoani Morogoro.

Ndege hiyo ilitambulishwa rasmi katika maonyesho ya kimataifa ya wazalishaji wa bidhaa za Viwandani Tanzania yajulikanayo kwa jina la Tanzania International Manufacturers Expo 2023 (TIMEXPO) yaliyomalizika hivi karibuni kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.

Akizungumzia hilo mmoja wa wakurugenzi wa kampuni hiyo, David Grolig amesema kuwa uamuzi wa kuzalisha  ndege hiyo umetokana na mazingira mazuri ya uwekezaji hapa nchini.

Grolig amesema kuwa ndege hiyo aina ya Skyleader 600 ina uwezo wa kubeba abiria wawili (akiwemo rubani) na inakidhi mahitaji ya wafanyabiashara wanaosafiri umbali mrefu.

Amesema kuwa walifanya utafiti wa kina ili kuelewa mahitaji ya wafabiashara ambao mara nyingi hufanya safari za masafa marefu na kutumia muda mwingi njiani.

Akifafanua zaidi amesema kuwa kutokana na utafiti huo, waliamua kutengeneza ndege itakayowawezesha wafanyabiashara kusafiri kwa urahisi zaidi na kuhudhuria mikutano mbalimbali nje ya mkoa kabla ya kurejea na kuendelea na shughuli nyingine.

“Tunajivunia kutengeneza ndege ya aina hii ambayo ni muhimu kwa wafanya kibiashara na watu binafsi. Huu ni mwanzo na mwakani tutatengeneza ndege nyingine aina ya Skyleader 500 ambayo ni muhimu kwa matumizi ya kilimo na shughuli zingine,” amesema

“Ndege zote hizi ni matunda ya ubunifu wa wataalamu wetu wazawa na wa kigeni, ambapo watalaamu wazawa wamepata mafunzo Jamhuri ya Czech na mipango ya kuendelea kutoa mafunzo inaendelea ili kuwa na wataalamu wengi zaidi,” amesema Grolig.

Amesema kuwa umiliki wa ndege hiyo ni rahisi zaidi na wamefanya hivyo ili kuendeleza gurudumu la uchumi kwa Watanzania na wateja wao wan je ya nchi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi mwenza wa kampuni hiyo, Igor Stratil, alisisitiza kuwa ndege hiyo Na.1 ni matokeo ya utaalamu wa pamoja ya timu ya Tanzania na Czech.

Stratil amesema pia wamefurahi kushiriki katika maonyesho ya TIMEXPO na kuwa washindi wa jumla.

Maonesho hayo yalifunguliwa rasmi na Waziri wa Elimu, Sayansi, na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, na kushirikisha ambapo jumla ya washiriki 138 washiriki na wageni zaid ya 1,000 walikuwa wanatembelea kila siku.

Miongoni mwa waliohudhuria ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, ambaye alifunga maonyesho hayo na kuwapongeza waandaaji na kampuni ya AAL kwa maendeleo ya sekta ya viwanda nchini.

Chalamila amesema kuwa ubunifu wa kutengeneza ndege ni kichochea maendeleo ya teknolojia na nyenzo pekee ya kuvutia wawekezaji wengine na kuchangia ustawi wa jamii.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here