Home KITAIFA BENKI YA MAENDELEO TIB YAWEKEZA BILIONI 334.7/- SEKTA YA KILIMO NCHINI

BENKI YA MAENDELEO TIB YAWEKEZA BILIONI 334.7/- SEKTA YA KILIMO NCHINI

Google search engine

*SEKTA YA MAJI YAMWAGIWA BILIONI 14, SASA YAWA CHEMICHEMI YA SOKO LA AJIRA

Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo- TIB, Lilian Mbassy, akizungumza leo Oktoba 16, 2023 katika kikao na Wahariri wa habari ulioratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina
Baadhi ya wahariri wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo- TIB, Lilian Mbassy (hayupo pichani)

Na MWANDISHI WETU

-BEST MEDIA, DAR ES SALAAM

BENKI ya Maendeleo ya TIB imefanikiwa kulifungua Taifa kwa kufanya uwezaji wenye tija ambapo kwa sasa imefanikiwa kuwekeza kiasi cha Sh bilioni 334.7 kwa ajili ya kusaidia sekta ya kilimo nchini.

Mbali na hatua hiyo pia benki hiyo imefanikiwa kufanya uwekezaji katika sekta ya nishati, maji ambapo hadi kufikia Septemba 30, 2023, imewekeza kwenye miradi ya jumla ya Sh Bilioni 980.7 sawa na asilimia 93 ya miradi ni ya sekta binafsi na asilimia 7 ya miradi ni ya sekta ya umma huku asilimia 80 ya miradi ni ya muda mrefu zaidi ya miaka mitano.

Akizungumza leo Oktoba 16, 2023 katika kikao na Wahariri wa habari ulioratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina, Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo- TIB, Lilian Mbassy, amesema kuwa pamoja na kuwa na mikakati Madhubuti ya kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa umma na wadau wa sekta binafsi lakini nyakati zote zimekuwa wakipata msaada wa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dk, Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha wanapata ruzuku ya Serikali kama njia ya kuimarisha ufanisi kwao.

Kutokana na hali hiyo Mbassy, amesema kuwa matokeo ya uwekezaji uliofanywa na benki hiyo kwenye miradi ya maendeleo imezingatia utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya Taifa ambapo jumla miradi 253 ya Sekta Kilimo, usindikaji wa mazao ya kilimo imekopeshwa Sh Bilioni 334.7 kiasi kilichowekezwa katika sekta ya kilimo na mikoa 23 na wilaya 76 zilizonufaika na uwekezaji huo.

“Zaidi ya wananchi 10,230 wamepata ajira katika sekta ya kilimo. Taasisi za kifedha 12, SACCOS 78 na Kampuni 128 zimekopeshwa,” amesema Mbassy

Kaimu Mkurugenzi huyo, amesema kuwa matokeo ya uwekezaji  katika Sekta ya Maji wamefanikiwa kutoa fedha katika miradi ya Maji 66 imekopeshwa (Mamlaka za Maji – 6 na Jumuiya za Watumia Maji Vijijini 60).

“Shilingi Bilioni 14.9 ni kiasi kilichowekezwa Sekta ya Maji na Usafi wa Mazingira. Mikoa iliyonufaika ni Dodoma, Singida, Shinyanga, Tanga, Mtwara, Iringa, Morogoro na Ruvuma. Jumla ya Wananchi 750,000 wamenufaika na miradi ya Maji, ambapo Kilomita 157 za Mtandao wa Usambazaji wa Maji zimefikiwa.

“Mifano ya baadhi ya miradi mikubwa ya kimkakati iliyowezeshwa na Benki ya Maendeleo TIB ni TPDC na Wentworth – miradi kwenye gesi asilia. TANESCO – mitambo ya usambazaji wa umeme wa msongo mkubwa (Somanga-fungu), NHC – mradi wa nyumba za makazi, Kagera Sugar Ltd – mradi wa kiwanda cha Sukari, Amiri Hamza Ltd – mradi wa kuchakata kahawa mkoani Kagera.

“Pia ipo CATA Mining Co. Ltd – mradi wa uchimbaji na uchenjuaji wa madini ya dhahabu. TTC – mradi wa uimarishaji wa miundombinu ya mawasiliano, Pipes Industries Co. Ltd -kuwezesha ujenzi na ununuzi wa mitambo na mashine za kufanyia kazi, Msagara Investment Company Limited – kuwezesha ununuzi wa laini ya uzalishaji wa ‘gauze’ pamba maalumu zinazotumika katika masuala ya upasuaji,” amesema Mbassy

Akizungumzia uwekezaji Uwekezaji uliofanywa na Benki umefanikiwa kugusa maeneo sita (6) ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ambayo ni katika kukomesha programu ya kukomesha njaa wamefanikiwa kutoa kiasi cha Sh Bilioni 334.7.

“Shilingi Bilioni 12kiasi kilichowekezwa nishati safi na nafuu. Mfano Miradi ya TANESCO TEDAP &TREEP na kwenye Ubora wa Elimu tumewekeza kiasi cha Shilingi Bilioni 14.8Mfano Vyuo vya TUDARCO na MUST. Maji Safi Usafi wa Mazingira Shilingi Bilioni 14.9ambapo fedha hizi tumetoa kupitia mamlaka za maji na jumuiya za watumia maji.

Kaimu Mkurugenzi huyo wa Benki ya Maendeleo TIB, amesema kuwa pamoja na hali hiyo pia zipo faida za uwekezaji uliofanywa ikiwamo kuongeza ajira kwa Watanzania walio wengi huku zaidi ya ajira 30,000 zimetokana na uwekezaji uliofanywa na benki pamoja na kuongeza mapato ya Serikali kupitia kodi na tozo mbalimbali.

“Kuongeza mapato ya fedha za kigeni kutokana na mauzo ya bidhaa nje ya nchi. Jumla ya Matrekta 249, ‘Combined harvesters 6’, na ‘Power Tillers’ 137 zimefadhiliwa kupitia Dirisha la Kilimo ikiwamo kurahisisha upatikanaji wa malighafi za viwanda na kuongeza uzalishaji wa bidhaa na kuondoa utegemezi wa bidhaa hizo kutoka nje ya nchi.

“Misaada kwa jamii kama ujenzi wa zahanati, madarasa na miundombinu. Mfano Kagera Sugar imejenga Zahanati ya Kisasa Wilayani Misenyi na Kampuni ya Amir Hamza (T) Ltd imejenga Barabara kwenye eneo la mradi. Kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama kwa kutibu maji kabla ya matumizi na kuboresha afya kutokana na matumizi ya maji safi na salama.

“Kuimarisha ufanisi wa makusanyo ya mauzo ya maji kupitia mfumo wa malipo kabla, matumizi ya umeme jua yanapunguza gharama za uendeshaji miradi ya maji katika jumuiya za maji vijijini kwa kuondoa gharama za kununua dizeli, matengenezo ya mara kwa mara ya genereta, na kupunguza gharama za usimamizi pamoja na kuzijengea jumuiya za maji utamaduni wa kuchangia na kukopa benki ili ziweze kujitegemea na kuipunguzia Serikali mzigo wa kuzihudumia,” amesema Mbassy

Huduma Nyingine Zinazotolewa na Benki

Akifafanua zaidi kuhusu huduma nyingine zitolewa na benki hiyo ikiwamo usimamizi wa mifuko ambapo ni moja ya jukumu la Benki ya Maendeleo TIB ni kusimamia fedha za uwakala.

“Fedha hizo zinasimamiwa na Benki kwa niaba ya Serikali na mawakala wa miradi ya maendeleo, miradi hii haipo kwenye mizania ya Benki (off balance sheet). Ambapo mpaka kufikia Septemba 30, 2023, benki inasimamia jumla ya mifuko 8 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 197.12,” amesema Kaimu Mkurugenzi huyo

Akizungumzia huduma mahususi za ushauri wa Kitaalamu, Mbassy, amesema kuwa Benki yao imetoa ushauri wa kitaalamu katika miradi ya kimkakati ikiwamo ATCL, TTCL ikiwamo utengenezaji wa mpango wa biashara wa muda wa kati.

“Kwa upande wa TPDC mradi wa utafutaji wa gesi (gas exploration) katika Bahari ya Hindi kupitia Kampuni ya M&P napo hapa tuliweza kuwahudumia kupitia mpango huu na kwa TANESCO kupitia mradi wa utanuzi wa huduma za umeme mijini.

“DART kupitia mpango wa kibiashara na fedha (commercial and financial structure), ushauri wa kitaalamu wa mradi wa DART, TPA mpango wa kibiashara na fedha (commercial and financial structure) kwa ajili ya mradi wa Bandari ya Bagamoyo, ushauri wa kitaalamu katika uendeshaji miradi ya Bandari ya Bagamoyo.

“Wengine ni TRL kupitia mpango wa kibiashara na fedha, ushauri wa kitaalamu wa miradi wa TRL, Mradi wa Bomba la Mafuta (EACOP)- Hoima (Uganda)-Tanga (Tanzania) na Mfuko wa Msaada wa Kiufundi.  Benki ya Maendeleo TIB hutenga fungu maalum kwa ajili ya kusaidia taasisi na mashirika kuandaa miradi inayokidhi vigezo vya uwekezaji na mikopo,” amesema

Amesema baadhi ya miradi iliyofaidika na mfuko huu ni pamoja na Mradi wa Kituo cha Mabasi Mbezi Louis (Magufuli Bus Terminal) kupitia Jiji la Dar es Salaam (DDC), Mradi wa Soko la Kisasa la Kisutu kupitia Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Mradi wa Kiwanda cha Kuchakata Zabibu kwenye eneo la Chinangali Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Dodoma,  Mradi wa Kituo Kikuu cha Kimataifa cha Mabasi Kinachojengwa eneo la Ngangamfumuni katika Manispaa ya Moshi na miradi ya soko la kisasa na kituo kipya cha mabasi cha Halmashauri ya Manispaa ya Lindi.

Kuhusu mradi wa Sekta ya Nishati, Mbassy amesema kuwa kupitia mradi  wa Upanuzi wa nishati ya umeme vijijini(Tanzania Rural Electrification Expansion Programme-TREEP), Benki inaendelea  kushirikiana na Benki ya Dunia kupitia REA, kutoa mikopo kwa wazalishaji wa nishati jadidifu wanaohudumia maeneo ya vijijini ambako umeme wa TANESCO haujafika.

“Kupitia mradi wa ‘’Waste to Energy’’ Benki itaendelea kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda (UNIDO), katika kuchochea matumizi ya ethano kama chanzo mbadala cha nishati safi na nafuu ya kupikia. Kuendelea kuwekeza TANESCO kwa Kushirikiana na taasisi zingine za fedha kwenye kufadhili miradi ya Umeme jua (Zuzu Solar PV) MW 50,” amesema

Pamoja na hali hiyo Kaimu Mkurugenzi huyo, amesema kuwa benki yao itaendelea na uwekezaji kwenye mamlaka za maji nchini.

“Benki inaendelea kufanya kazi na taasisi za Serikali na Jumuiya ya Maendeleo kama KfW, GiZ, IFF/OBA, Mfuko wa Maji wa Taifa (NWF), Benki ya Dunia na washirika wengine wenye nia ya kuwekeza katika sekta ya maji.

“Kupitia Sekta ya Kilimo kwa kuwa na Dirisha la Kilimo lenye riba nafuu ya asilimia 4 hadi 5, benki itaendelea kuwekeza katika shughuli za mnyororo wa thamani katika kilimo kuanzia shughuli za awali hadi usindikaji wa mazao ni eneo la kimkakati la benki. Pamoja na kuwa na miradi katika sekta mbalimbali ikiwamo uwekezaji kwenye Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwenye miradi ya ujenzi wa makazi na uwekezaji kwenye miradi ya Ukarabati wa meli chini ya Kampuni ya Huduma za Meli,” amesema

SAFARI BENKI ILIPOANZIA

Benki ya Maendeleo TIB, mwanzo ilijulikana kama Benki ya Uwekezaji Tanzania, TIB, ni benki ya maendeleo inayomilikiwa na serikali nchini Tanzania. Benki hiyo ni taasisi ya kwanza ya fedha ya maendeleo iliyoanzishwa na Serikali ya Tanzania. Shughuli za TIB zinasimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania, benki kuu na mdhibiti wa kitaifa wa benki. TIB imesajiliwa kama Taasisi ya Fedha Iliyosajiliwa

Benki ya Maendeleo TIB (iliyokuwa inajulikana kama Tanzania Investment Bank) ilianzishwa kama Taasisi ya Fedha ya Maendeleo (Development Finance Institution – DFI) kwa mujibu wa Sheria namba 20 ya mwaka 1970 iliyopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tarehe 6 Novemba, 1970 ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kujenga Taifa linalojitegemea kwa kutumia rasilimali zake. Kwa mujibu wa sheria hiyo, “maendeleo ya kiuchumi”

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here