Home KITAIFA KISHINDO CCM, MABADILIKO MAKUBWA YATARAJIWA LEO

KISHINDO CCM, MABADILIKO MAKUBWA YATARAJIWA LEO

Google search engine

Na MWANDISHI WETU

-DODOMA

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, leo huenda akaiomba Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) iridhie kufanyika kwa mabadiliko ya watendaji ndani ya chama.

Hatua hiyo inatajwa kuwa huenda ikaleta kishindo hasa kwa Sekreterieti ya chama hicho tawala kubadilika kama njia ya kupanga safu ya mashambulizi kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu mwaka 2025.

Taarifa za ndani kutoka CCM zinaeleza kwamba wakati wajumbe wakianza kuingia ukumbini kwa ajili ya kupokea taarifa za kikao, tayari Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Sophia Mjema ambaye alikuwa Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi na kumteua kuwa Mshauri wa Rais Masuala ya Wanawake na Makundi Maalum, hatua ambayo inatajwa huenda ikaleta sura mpya kwenye idara hiyo nyeti ndani ya CCM.

Mbali na hao pia wanasiasa wakongwe ambao wamekuwa wakitajwa katika mabadiliko hayo kuwa huenda sura yake ikachomoza ni aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Misri na Brazil, Dk. Emmanuel Nchimbi.

Dk. Nchimbi ambaye pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Vijana wa CCM Taifa ameshika nafasi mbalimbali ikiwamo Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM (CC) kwa nyakati tofauti.

“Tunaingia kikao lakini leo inaweza kutokea mtikisiko mkubwa ndani ya chama kwa kuwa na sura mpya za kazi. Unajua CCM ni kiwanda kikubwa na kitovu cha siasa za Tanzania. Yapo mengi ya taarifa za Serikali katika masuala mbalimbali na pia tunataraji kupokea mapendekezo ya uteuzi mpya wa watendaji.

“Kama yapo acha kwanza twende kikaoni na utaratibu wa CCM nyie kama wana habari mtapewa taarifa za kina kama ulivyo utaratibu wa CCM,” amesema mmoja wa wajumbe wa NEC ambaye hakutaka kutajwa jina lake.

Mbali na hilo majina ya wana CCM wengine ambao wamekuwa wakitajwa huenda wakaingia kwenye Sekreterieti mpya ni pamoja na na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila.

Chamila ambaye pia amewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, anatajwa kukijua chama hicho na amekuwa na utendaji ambao umesaidia kumpa namfasi mbalimbali ndani ya CCM ikiwamo kuwa Mjumbe wa Kamati ya Uhakiki wa Mali za CCM iliyokuwa inaongozwa na Dk. Bashiru Ally.

Google search engine

2 COMMENTS

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here