Home KITAIFA RAIS SAMIA: HAIKUWA RAHISI KUFIKIA MAKUBALIANO MKATABA TPA, DP WORLD

RAIS SAMIA: HAIKUWA RAHISI KUFIKIA MAKUBALIANO MKATABA TPA, DP WORLD

Google search engine

*ASEMA MKATABA UMEZINGATIA MAONI YA KILA UPANDE, BANDARI NI HIDAYA KWA TAIFA, SASA WAFANYAKAZI RUKSA KUBAKI TPA AU KWENYE DP WORLD

*MKURUGENZI TPA ASISITIZA SASA UFANISI UTAONEKANA BANDARI

Rais Samia Suluhu Hassan, akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini wa makubaliano wa uendeshaji wa Bandari kati ya Serikali na Kampuni ya DP World leo Ikulu ya Chamwino Jijini Dodoma

Na MWANDISHI WETU

-DODOMA

RAIS Samia Suluhu Hassan, amesema  kuwa haikuwa rahisi kufikia makubaliano haya lakini walisikiliza na kufuatilia maoni na hoja za kila mtu hivyo hakuna kundi au sauti ambayo imepuuzwa ambao Serikali iliunda jopo la wataalam kufuatilia maoni hayo.

Kauli hiyo ameitoa leo Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma, wakati wa utiaji Saini mikataba baina ya Serikali na Kampuni ya DP World kwa ajili ya uendeshaji wa Bandari ya Dar es Salaam.

Kutokana na hali hiyo Rais Samia, amewashukuru Watanzania wote waliotoa maoni kwani kazi hiyo ilifanywa vizuri na timu ya majadiliano ya wataalam na hakuna maoni yaliyoachwa hadi kufikia hatua hiyo muhimu kwa Taifa.

“Hakuna kundi au sauti ambayo imepuuzwa kwa kuangalia hoja zote, kazi hiyo ilifanywa vizuri sana na wale ambao ni wataalamu wa masuala ya kodi za Serikali tuliwajumuisha. Lakini katika jambo jipya ni lazima kutokee maoni tofauti nah ai hapa tulipofika ni sehemu ya yale tote ambayo watanzania wameyatoa.

“Bandari ni kiunganishi kati ya nchi yetu na mataifa mengine na hatua hii inakwenda kuongeza mapato ya Serikali na kuongeza ufanisi katika shughuli za kiuchumi. Tunaendelea kuwakaribisha wawekezaji zaidi katika Taifa letu.

“Na mikataba hii iliyosainiwa imezaliwa katika yale makubaliano ya awali lakini pia ninalishukuru Bunge kwa kupitia Azimio lakini pia na Baraza la Mawaziri kwa kuridhia na kungazia sheria zote ikiwamo ile ya Manunuzi. Nimpongeza Waziri wa Uchukuzi Profesa Mnyaa Mbarawa, timu ya majadiliano, Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa ushirikiano wake maana kila wakati tulikuwa tunamgongea mlango na hata kumwambia go and check,” amesema Rais Samia

Kwa ujumla na kipekee Rais Samia amewashukuru Watanzania wote waliotoa maoni kwani linapokuja jambo jipya ni lazima watu wawe na maoni tofauti.

Kutokana na hali hyo amewakaribisha watu wengi zaidi kuja kuwekeza Tanzania ili kuinua uchumi na kupunguza umaskini wa watu.

“Mawazo ya wawekezaji wa ndani kupewa bandari ni mazuri na ya kizalendo lakini yapo mbali na uhalisia. Katika kusiani mkataba huu, maslahi mapana ya nchi yamezingatia maslahi mapana ya nchi,” amesema

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Plasduce Mkeli Mbossa

Awali akitoa maelezo katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Plasduce Mkeli Mbossa​, amesema kuwa uwekezaji huo wa Serikali kupitia TPA utaongeza ufanisi kwa huduma za meli na shehena, kupunguza muda kwa bandari katika kuchakata nyaraka.

Pia utaongeza mapato ya serikali, kupungua kwa udanganyifu, kuimarisha nafasi ya ushindani kwa bandari, kuongeza ajira na kupunguza gharama za usafirishaji wa mizigo kuja bandari ya Dar es salaam.

Aidha amesema kuwa muda wa usafirishaji wa mizigo kutoka mashariki ya mbali utapungua kutoka siku 30 hadi 15.

“Haitegemewi na hatotokea kufungwa kwa biashara zozote za wazawa zinazofanyika bandarini,” amesema Mbossa

Aidha, Mbossa amesema kuwa wastani wa meli kukaa nangani ikisubiri huduma ni siku 5 hadi 10 huku bandari ya Mombasa ni siku 1.25 na Bandari ya Durban ikiwa ni wastani wa siku 1.6.

“Hii inatokana na kukosekana kwa uwekezaji mkubwa wa muda mrefu ambao ungepelekea kuongezeka kwa namba za gati. Pia gharama za kusafirisha makasha ni kubwa, jambo linalofanya kupanda kwa bei ya bidhaa kwa mtumiaji wa mwisho,” amesema

Amesema kuwa mikataba inayosainiwa leo ni baina ya nchi mwenyeji, mkataba wa ukodishaji na uendeshaji wa gati namba 4-7 lakini pia kutakuwa na sehemu ambayo gati 0-3 zitaendeshwa kwa ushirikiano wa pamoja kati ya TPA na kampuni ya DP World kwa shughuli za kibiashara na shughuli za kiserikali.

Amesema kuwa mikataba hiyo, haihusishi eneo lote la bandari wala bandari zingine za Tanzania, ambapo kwa upande wa gati namba 8-11, mchakato wa kumpata mwendeshaji mwingine umeshaanza kufanyika na akipatikana mwekezaji mwingine mwenye sifa atakabidhiwa na sio DP World.

“Katika mikataba hii, Serikali itakuwa inapata ada na tozo kutoka DPW ambazo zitaongeza mapato na kupunguza gharama za uendeshaji,” amesema

MKATABA WA MIAKA 30

Amesema kuwa mkataba huo utakuwa wa miaka 30 na utendaji kazi wa DPW utakuwa unapimwa kila baada ya miaka mitano  na sio miaka 100.

Aidha amesema kuwa watumishi wa sasa wa TPA watakuwa na nafasi ya kuchagua kati ya kubaki TPA au kuhamia kampuni ya DPW.

“Pia, mwekezaji atalipa kodi zote za Tanzania kwa mujibu wa Sheria za Tanzania, sheria za Tanzania ndio zitatumika katika kutekeleza mkataba huu na serikali itakuwa na haki ya kujiondoa kwenye mkataba ikiona inafaa,” amesema

Bandari zetu zinaendeshwa katika hali ya ushindani kama zilivyo bandari nyingine duniani. Mazingira hayo yanachagizwa na mabadiliko ya ukuaji wa sekta ya usafirishaji majini, teknolojia na ukuaji wa uchumi. Hivyo, TPA kama Taasisi iliyokasimishwa jukumu la umiliki, uendeshaji, uendelezaji na usimamizi wa Bandari nchini ina jukumu la kutoa huduma sambamba na kasi ya mabadiliko hayo.

Amesema Katika kuendana na kasi ya mabadiliko hayo, moja ya mikakati ambayo imebainishwa katika Mpango Kabambe wa Uendelezaji wa Bandari Tanzania wa mwaka 2009 ambao ulifanyiwa marejeo mwaka 2022, umetoa mapendekezo kwa Serikali kuhusu namna ambayo inaweza kufikia azma yake ya TPA kuwa Mmiliki na/au Mwendelezaji wa bandari nchini na kukasimisha shughuli za uendeshaji kwa Sekta Binafsi ili kuongeza ufanisi wa Bandari za Tanzania.

“Pamoja na kuchukua hatua mbalimbali za maboresho ya Bandari ya Dar es Salaam, bado ufanisi katika utoaji huduma za bandari haujafikia viwango vinavyotakiwa kimataifa. Hali ya sasa ya utendaji wa Bandari ya Dar es Salaam imeendelea kuwa ya kiwango cha chini ikilinganishwa na bandari shindani kikanda. Kwa mfano, meli nyingi husubiri nangani kwa muda mrefu kabla ya kuhudumiwa. Leo hii, kuna meli 30 zilozofika bandarini (nangani) zikisubiri kuingia bandarini kushusha mizigo wakati zile zinaazohudumiwa gatini ni jumla la meli 11. Wastani wa meli kusubiri nangani kwa Bandari ya Dar es salaam ni siku 5 ikilinganishwa na siku 1.25 kwa Bandari ya Mombasa na siku 1.6 kwa Bandari ya Durban.

“Ufanisi huu mdogo wa Bandari ya Dar es Salaam umetokana na changamoto mbalimbali zikiwemo: kukosekana kwa mifumo ya kisasa ya TEHAMA ambayo haiwezi kusomana; kutokuwepo kwa maeneo ya kutosha ndani na nje ya bandari kwa ajili ya kuhifadhia shehena ya mizigo pamoja na uchache wa magati au maegesho ya meli; na kukosekana kwa mitambo ya kutosha na ya kisasa ya kuhudumia shehena ambayo teknolojia yake inabadilika mara kwa mara na ina gharama kubwa ya uwekezaji na uendeshaji,” amesema Mbossa

ATHARI YA KUTOKUWA NA UFANISI

Mkurugenzi huyo wa TPA, amesema kuwa athari za kutokuwa na ufanisi katika Bandari ya Dar es Salaam ni pamoja na: meli kusubiri muda mrefu nangani ambako kunasababisha kuongezeka kwa gharama ya kutumia bandari ya Dar es Salaam, kwa mfano gharama za meli kusubiri nangani kwa siku moja ni takriban Dola za Marekani 25,000, sawa na takriban Shilingi milioni 58 kwa siku, meli kutumia muda mrefu kupakia na kupakua shehena gatini kwa wastani wa siku 5 ikilinganishwa na siku 1 inayokubalika kimataifa; meli kubwa kutokuja katika bandari ya Dar es Salaam kutokana na kuchukua muda mrefu kuhudumiwa.

Amesema hali hiyo, husababisha bandari yetu kuwa bandari inayolishwa shehena na bandari nyingine (feeder port) na hivyo kuongeza gharama ya kutumia bandari hiyo na kuikosesha nchi mapato ambayo yangeweza kutumika katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati nchini ambayo ingesaidia kukuza uchumi na kuboresha huduma za wananchi.

“Pia, hali hii ya kukosekana kwa ufanisi inaongeza gharama katika mnyororo mzima wa usafirishaji (total route costs) kutoka nje ya nchi, kupitia katika bandari yetu kwenda nchi za jirani zinazotumia bandari hiyo ya Dar es Salaam. Kwa mfano, gharama ya kusafirisha kasha moja kutoka nje ya nchi (on transit) kwenda nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zinafikia takriban Dola za Marekani 12,000.

“Hii ni gharama kubwa sana ikilinganishwa na Bandari shindani za Mombasa, Beira, Maputo na Durban ambazo ni wastani wa nusu ambazo zinatumika kwa kutumia bandari ya Dar es Salaam. Gharama za usafirishaji kwa mizigo ya ndani ni takribani Dola za Marekani 6,000 kwa kasha ambazo zinapelekwa kwa mlaji wa mwisho ambaye ni mwananchi wa kawaida. Gharama za kupitisha mzigo kama huo kwa bandari jirani ya Mombasa ni takribani Dola za Marekani kati ya 3,500 hadi 4,000,” amesema

Mbossa amesema kwa kutambua kuwa Serikali pekee haitaweza kutatua changamoto zilizopo kwenye Bandari ya Dar es Salaam, kuanzia miaka ya 2000, Serikali ilianza  kushirikisha sekta binafsi na iliingia mkataba wa upangaji na uendeshaji (lease and concession agreement) na Kampuni ya Kimataifa ya Uendeshaji wa Vitengo vya Makasha, Hutchison ya Hong-Kong China kupitia Kampuni ya TICTS.

Amesema mkataba huo ulidumu kwa miaka ishirini na mbili (22) kuanzia mwaka 2000 hadi mwaka 2022 na kampuni hiyo ya TICTS ilipewa haki ya kipekee ya kuendesha shughuli za kuhudumia makasha katika gati namba 8 hadi 11 za Bandari ya Dar es Salaam. Wakati huo huo TPA iliendelea kuendesha na kuhudumia maeneo mengine ya Bandari hiyo ya gati namba 0 hadi 7 pamoja na magati ya mafuta ya KOJ na SBM.

Amesema makampuni mengi yamekuwa yakionesha nia ya kuendesha bandari ya Dar es Salaam lakini TPA iliingia makubaliano na Kampuni ya DP World kutokana na uzoefu wake katika uendeshaji wa shughuli za bandari barani Afrika, Asia, Ulaya na Amerika ya Kaskazini na Kusini. Kampuni hiyo pia, ina utaalamu wa kuchagiza mnyororo mzima wa usafirishaji (end to end total logistics chain solution) kutoka maeneo ambayo bidhaa zinatoka mpaka kufika kwa Walaji.

“Pia, uendeshaji wa maeneo maalum ya kiuchumi (special economic zones) karibu na bandari, usafirishaji baharini na  nchi kavu (kupitia njia ya reli), uwekezaji mkubwa katika maeneo mbalimbali ambayo imewekeza pamoja na kuajiri Wazawa katika maeneo hayo.

“Kwa upande wa makampuni mengine ambayo yaliwasilisha mapendekezo yao yalionesha nia ya kuwekeza bandarini pekee na sio kuchagiza mnyororo mzima wa usafirishaji na kutafuta masoko ya kimkakati katika eneo la usafirishaji wa shehena ya mizigo. Pia, baadhi ya makampuni hayo hayana uzoefu wa kuendesha shughuli za bandari barani Afrika wakati Kampuni ya DP World inaendesha takriban bandari sita (6) barani Afrika na bandari zaidi ya 68 duniani kote kwa ufanisi mkubwa.

“Katika kutekeleza mikakati ya Serikali ya kuimarisha shughuli za bandari ya Dar es Salaam; muda mfupi ujao utashuhudia utiaji saini wa mikataba mitatu (3) ya uwekezaji na uendeshaji wa bandari ya Dar es Salaam ambayo ni: Mkataba wa Nchi Mwenyeji, Mikataba ya Ukodishaji na Uendeshaji wa Gati Namba 4 hadi 7 za bandari ya Dar es Salaam.

“Aidha, Gati Namba 0 hadi 3 za bandari ya Dar es Salaam zitatumiwa kwa pamoja baina ya Kampuni ya DP World na Serikali kupitia TPA kwa ajili ya shughuli zingine za kibiashara na Serikali. Naomba kusisitiza kwamba, mikataba hii haihusishi eneo lote la bandari ya Dar es Salaam na bandari nyingine za Tanzania.

“Naomba kukutaarifu kwamba, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania imeanza mchakato wa kumpata mwekezaji wa ndani au wa nje kwa ajili ya kuendesha Gati Namba 8 hadi 11.

“Mheshimiwa Rais, Katika Mikataba hiyo mitatu (3), Serikali itakuwa ikipokea ada na tozo kutoka kwa Kampuni ya DP World ambazo zitaongeza mapato yake na kupunguza gharama za uendeshaji. Hapo awali, Serikali ilikuwa inatumia takribani asilimia 90 ya mapato yaliyokusanywa katika uendeshaji wa maeneo hayo yaliyokodishwa na kubakiwa na asilimia 10 tu ya mapato yote. Hivyo, kutokana na Mikataba hii, Serikali itaweza kubaki,” amesema

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here