Home KITAIFA WANAHABARI WATAKIWA KUTANGAZA MATOKEO YA SENSA KWA LUGHA RAHISI

WANAHABARI WATAKIWA KUTANGAZA MATOKEO YA SENSA KWA LUGHA RAHISI

Google search engine
Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, Spika Mstaafu Anne Makinda, akizungumza na wanahabri (hawapo pichani), pia akiwa katika ukumbi huo alikuwa akibadilishana mawazo na viongozi wa Sensa kutoka Zanzibar katika mafunzo ya waandishi wa habari yaliyofanyika jijini Arusha

Na Jane Edward

-Arusha

Wanachama wa vilabu vya waandishi wa habari kutoka Kilimanjaro, Manyara na Arusha wametakiwa kutumia taaluma waliyonayo kuelezea matokeo ya sensa ya watu na makazi iliyofanyika mwaka 2022 hapa nchini.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela, katika mafunzo ya siku mbili yaliyo wakutanisha wataalamu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), yanayofanyika kwa siku mbili jijini Arusha.

Mongela amesema kuwa waandishi wa habari ni sekta muhimu katika kutoa elimu kwa jamii juu ya namna sensa ilivyo fanyika vizuri na kwa uwazi na kuelezea matokeo ya sensa hiyo kwa upana wake.

“vyombo vyetu vya habari viandae mijadala inayohusu matokeo ya Sensa ili kupanua upeo wa wananchi katika kuangalia maswala ya maendeleo kwa wananchi wetu “Alisema Mongela

Amesema kuwa Lengo la Serikali ni kuona matokeo ya Sensa yanawafikia wadau wote hususani wananchi ili waweze kuyatumia katika shughuli zao binafsi na pia kuzitumia katika kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya nchi ikiwemo kushiriki katika kupanga, kufuatilia na kutathmini shughuli za maendeleo zinazotekelezwa na Serikali .

 Aidha amesema kama ilivyokuwa kwa  wakati wa kuhamasisha wananchi kushiriki Sensa, hivi sasa ni wakati wa kuyawasilisha kwa wananchi kwa lugha rahisi na kwa weledi kupitia taaluma ya habari.

Awali wakati wa kumkaribisha mgeni Rasmi Kamisaa wa sensa na spika mstaafu Anna Semamba Makinda amesema sensa ya mwaka huu imefanikiwa kwa asilimia 99.99 ambapo takwimu hizo za sensa zinakubalika na kuaminika Duniani.

Amesema mategemeo yake ni kuona waandishi wanafahamu masuala ya takwimu na kutumia lugha rahisi katika uandishi wao ili wananchi waweze kuelewa.

Amesema katika matumizi ya takwimu kwa waandishi wa habari itawasaidia katika taarifa zao mbalimbali kwa kuwa huwa hazidanganyi na kuwataka waandishi wasifanye kazi kwa hofu.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here