Home KITAIFA DK. MPANGO: SERIKALI INATAMBUA ‘VITA’ KWENYE UJENZI VIWANDA VYA DAWA NCHINI

DK. MPANGO: SERIKALI INATAMBUA ‘VITA’ KWENYE UJENZI VIWANDA VYA DAWA NCHINI

Google search engine
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Philip Mpango akizungumza na wafanyakazi wa Kiwanda cha MSD cha kutengeneza Mipira ya Mikono (Gloves) pamoja na wananchi mbalimbali wa mji wa Makambako mara baada ya kuweka Jiwe la Msingi katika kiwanda hicho kilichopo Makambako mkoani Njombe. (tarehe 26 Oktoba 2023).
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Philip Mpango akisikiliza maelezo kutoka kwa mkuu wa mradi wa kiwanda cha Mipira ya Mikono (Gloves), Selwa Hamid kuhusu maendeleo ya kiwanda wakati akitembelea na kukagua shughuli mbalimbali zinazofanyika katika Kiwanda cha MSD cha kutengeneza Mipira ya Mikono (Gloves) kilichopo Idofi, Makambako mkoani Njombe. (tarehe 26 Oktoba 2023)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Philip Mpango akitembelea na kukagua shughuli mbalimbali za uzalishaji zinazofanywa katika Kiwanda cha MSD cha kutengeneza Mipira ya Mikono (Gloves) kilichopo Idofi, Makambako mkoani Njombe. (tarehe 26 Oktoba 2023)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Philip Mpango akisalimiana na viongozi mbalimbali wakati alipowasili katika Kiwanda cha MSD cha kutengeneza Mipira ya Mikono (Gloves) kilichopo Idofi, Makambako mkoani Njombe. (tarehe 26 Oktoba 2023)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Philip Mpango akiweka Jiwe la Msingi katika Kiwanda cha MSD cha kutengeneza Mipira ya Mikono (Gloves) kilichopo Idofi, Makambako mkoani Njombe. (tarehe 26 Oktoba 2023)

Na MWANDISHI WETU

MAKAMU wa Rais Dk. Philip Mpango, amesema serikali inatambua vita iliyopo katika ujenzi wa viwanda vya dawa lakini kwa kuwa uwamuzi huo ni wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan hakuna atakayefanikiwa kuvikwamisha hivyo vitajengwa.

Amesema kwa sasa Serikali inaagiza dawa kwa asilmia 80 na vifaa tiba kwa asilimia 90 kutoka nje ya nchi, hali inayosababisha uhaba wa vifaa na gharama kubwa za uagizaji wa vifaa vya afya hivyo ni lazima kuchukua maamuzi magumu.

Akizungumza mkoani Njombe leo Oktoba 26, 2023, wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Kiwanda cha Mipira ya Mikono (Gloves) kinachosimamiwa na Bohari ya Dawa (MSD), Makamu wa Rais Dk. Mpango amesema Serikali inatambua vita iliyopo katika ujenzi wa viwanda hivyo vya dawa.

Amesema kuwa Rais Dk. Samia, ameamua hivyo viwanda hivyo vitajengwa kwa gharama yeyote kwa kuwa nchi ina uhaba  wa dawa na vifaa tiba.

“Bidhaa hizo zinaagizwa kutoka nje dawa zinaagizwa kwa asilimia 80 na vifaa tiba kwa asilimia 90 tumeamua kuipatia MSD majukumu manne ambayo ni uzalisha, ununuzi, utunzaji niwahakikishie viwanda hivi vitajengwa.

“Ujenzi wa viwanda hivi umelenga kuongeza upatikanaji wa dawa na vifaa tiba, kupunguza matumizi fedha za kigeni, uhaba wa dawa, gharama kubwa kuagiza bidhaa hizo na kutoa ajira,” amesema.

Kutokana na hali hiyo, Dk. Mpango, amesifu hatua ya utekelezaji wa mradi huo ambao kwa sasa umefikia asilimia 90 kutoka asilimia 30 ambapo Rais Samia alikuta ujenzi ambao umekamilishwa na wataalamu wa ndani kwa kushirikisha mamlaka husika.

“Uwepo wa kiwanda hiki ni muhimu sana kwa ajili ya mahitaji ya ndani na nje ya nchi wakati wa Corona tulihangaika sana matumizi ya gloves ni makubwa kiwanda hiki ni mkombozi hivyo lengo la Rais Dk. Samia lazima lifikiwe,” alisisitiza.

Ameongeza kuwa Serikali itaendelea kuwezesha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba.

Dk. Mpango amesema, wapo katika mkakati wa kuiongezea mtaji MSD ili kujenga viwanda na maghala na kuongeza upatikanaji wa dawa na vifaa tiba.

“Nataka uzalishaji wa kiwanda uanze mara moja Januari  mosi  mwaka 2024 na kiwanda hiki hakitoki hapa kitabaki, kitazalisha niwaagize  MSD ongezeni uzalishaji mwingine wa maji tiba na vitendanishi na kampuni Tanzu ya MSD zingatieni misingi ya kibiashara na watumishi zingatieni uzalendo.

“Pia niliagiza na nasisitiza tena watumishi wote wafanyiwe veting wale wanaotumiwa na wafanyabiashara kwa maslahi ya mifukoni mwao tuchukue hatua, ukipewa dhamana katika taasisi za umma zingatia maadili,” amesema

Dk. Mpango alieleza kuwa, ameteta na Rais Dk. Samia akiwa katika tukio hilo na kuagiza Tawala za Mikoa na Serikaliza Mitaa (TAMISEMI), kupitia Wakala  wa Barabara Vijijini wafanye tathimini ya ujenzi wa barabara ya kwenda katika kiwanda hicho ambayo inahitaji bilioni 1.4  ili ijengwe kwa kiwango cha lami.

“Hiyo ndio salamu ya Rais mimenong’ona naye hapa hapa kasema hashindwi kujenga barabara hii hivyo nawapa wiki mbili TAMISEMI malizeni tathimini ujenzi uanze,” amesema.

Pamoja na hali hiyo aliiagiza Wizara ya Fedha kuhakikisha fedha zilizotengwa kupunguza deni la MSD zitolewe haraka iwezekanavyo ili wasiendelee kulialia.

Awali akitoa taarifa ya utangulizi kwa Makamu wa Rais, Naibu Waziri wa Afya, Dk. Godwin Molel amesema kuwa wizara inatambua mapinduzi makubwa yanayofanywa na Rais Dk. Samia na serikali yake katika kuleta mapinduzi sekta ya viwanda hususani vya dawa.

Kutokana na hali hiyo aliahidi wizara itahakikisha hakuna kinachokwama na kiwanda hicho kitaanza uzalishaji mbali na vita kubwa iliyopo.

“Tutatoka salama Waziri Ummy atahakikisha kiwanda hiki kinazalisha, tunajua vita ni kubwa changamoto ni nyingi, tutashirikiana na bunge na taasisi nyingine tutakwenda,” amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Mavere Tukai amesema kiwanda hicho kimeanza uzalishaji wa awali na kinatararajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.

Amesisitiza kiwanda hicho kitasaidia kukuza uchumi na ndani ya miaka minane kitarudisha faida ambapo kwa mwaka wa kwanza faida itakuwa ni zaidi ya bilioni moja na ajira 200 kwa moja kwa moja na za muda.

Amesema kiwanda cha mipira ya mikono (gloves) Idofi hadi kikamilike kitagharimu Shilingi Bilioni 22.5, baada ya kukamilika kwa ujenzi na ufungaji wa mitambo, kiwanda hiki kitakuwa na uwezo wa kuzalisha mipira ya mikono 20,000 kwa saa sawa na jozi(pairs) 10,000 na hivyo kufanya uzalishaji wa takribani jozi 86,400,000 kwa mwaka.

“Hii ni sawa na asilimia 83.4 ya makadirio ya mahitaji ya mipira ya mikono nchini ya jozi milioni 104 kwa mujibu maoteo ya uhitaji ya bidhaa za gloves nchini kwa mwaka 2023/2024,” amesema.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here