Home KITAIFA WATANZANIA WAWILI HAWAJULIKANI WALIPO NCHINI ISRAEL

WATANZANIA WAWILI HAWAJULIKANI WALIPO NCHINI ISRAEL

Google search engine
Picha zikionyesha majengo yaliyolipuliwa Uganda wa Gaza (Photo by Ahmad Hasaballah/Getty Images)

Na MWANDISHI WETU

-DAR ES SALAAM

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inazo taarifa za kupotea kwa Watanzania wawili nchini Israel ambao ni miongoni mwa vijana 260 waliopo nchini humo kwa mafunzo ya kilimo cha kisasa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyolewa leo Oktoba 26, 2023 na Wizara ya Mambo Nje na Ushirikiano wa Afrika, Mashariki ilieleza kuwa Serikali kwa kushirikiana na Mamlaka mbalimbali nchini Israel inaendelea na juhudi za kuwapata vijana hao ili kuwaleta katika mazingira salama. Familia za vijana hao zimejulishwa kuhusu jitihada hizo na Serikali inaendelea kuwasiliana nao.

Watanzania 9 wanaoishi nchini Israel waliitikia wito wa mpango wa Serikali wa kuwarejesha nyumbani na walipokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, tarehe 18 Oktoba 2023.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here