*HALIMA MDEE ACHAMBUA MAOFISA MAENDELEO WALIVYOCHNGIA KUTOA MIKOPO HEWA YA HALMASHAURI
KAMATI ya kudumu ya Bunge ya hesabu sa serikali za mitaa (LAAC), imesema imebaini uwepo wa vikundi hewa vilivyopewa mikopo ya Shilingi milioni 895.94 kwenye baadhi ya halmashauri nchini.
Akitoa taarifa ya kamati kuhusu ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa hesabu zilizokaguliwa za mamlaka za serikalli za mitaa kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2022 leo Novemba 2, 2023 Bungeni Jijini Dodoma Mwenyekiti wa kamati hiyo Halima Mdee amesema kuwa
“Wakati wa majadiliano na Halmashauri mbalimbali, CAG aliifahamisha Kamati kuwa, baadhi ya halmashauri zilishindwa kuthibitisha uwepo wa baadhi ya vikundi,mfano wa halmashauri hizo ni H/M Kahama ambayo ilishindwa kukusanya mkopo wa Shilingi 133,752,600 kwa vikundi ambavyo havijulikani vilipo.
“Kwa upande wa H/Jiji Dar es Salaam, CAG alipohitaji kufanya uhakiki wa vikundi vilivyopewa mikopo, hakufanikiwa kukutana na vikundi 34 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu vilivyopewa mikopo ya jumla ya Shilingi 698,700,000 kutokana na kutokuwepo kwa vikundi hivyo, 2.8.6 fedha za Mikopo ya Vikundi kugawanywa miongoni mwa wanavikundi Shilingi Milioni 774.66,” amesema
Aidha, Mdee amesema katika kufuatilia matumizi ya fedha zilizotolewa kwa vikundi, Kamati imebaini udhaifu katika usimamizi wa mikopo inayotolewa katika vikundi mbalimbali kwa wana kikundi kugawana fedha za mkopo na hatimaye kushindwa kurejesha mkopo huo.
“Mheshimiwa Spika, ni dhahiri kuwa, kutowajibika kwa Wakurugenzi, Kamati ya mikopo na maafisa maendeleo ya jamii, kumesababisha hasara kubwa kwa taifa kama ambavyo tumeainisha hapo juu,”amesema
Amesema kwa kuwa uendeshaji usiofaa wa mfuko wa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu “kumekuwepo kwa kutozingatiwa kwa kanuni za usimamizi na utoaji wa mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu;
“Ukiukwaji wa kanuni hiyo umesababisha lengo la utoaji wa mikopo hiyo kwa jamii lisifikiwe; Kwa hiyo basi , bunge linaazimia kwamba:
“Kila halmashauri ichangie asilimia 10 ya mapato yake ya ndani kwenye mfuko wa wanawake, vijana na Watu wenye ulemavu na kuhakikisha kiasi kilichohojiwa cha Shilingi Bilioni 5.06 kinapelekwa katika mfuko huo”,