Home KITAIFA DK. BITEKO ASHIRIKI MAZISHI YA KAKA WA WAZIRI MKUU MAJALIWA

DK. BITEKO ASHIRIKI MAZISHI YA KAKA WA WAZIRI MKUU MAJALIWA

Google search engine
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Dotto Biteko akiweka udongo kwenye kaburi la kaka wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo, wilayani Ruangwa mkoani Lindi
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa na viongozi wa dini wakati wa swala la jeneza katika msiba wa kaka yake, ambeye amezikwa leo
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wananchi na viongozi mbalimbali waliofika kijijini kwao wilani Ruangwa katika msiba wa kaka yake ambaye amezikwa leo
Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, akitoa salamu za pole katika msiba wa kaka wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo, Novemba 6, Wilayani Ruangwa mkoani Lindi
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Dotto Biteko, akitoa salamu za pole kwa wafiwa katika msiba wa kaka wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ambaye amezikwa leo wilayani Ruangwa mkoani Lindi

Na MWANDISHI WETU

-LINDI

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko leo Novemba 06, 2023 ameongoza Viongozi mbalimbali wa Serikali katika mazishi ya Mzee Issa Nangalapa ambaye ni kaka wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Wilaya ya Ruangwa, Lindi.

Akizungumza katika ibada ya mazishi Dk. Biteko amempa pole Waziri Mkuu Majaliwa na kwamba ujio wa viongozi katika msiba huo ni ishara ya upendo walio nao kwake.

“Sisi ni kielelezo kuwa Watanzania wanaupendo nawe ndio maana tumekuja kuungana pamoja na wewe, kulia pamoja na wewe lakini kukutia moyo kwamba sisi tuliofika hapa na wengine tunakupa pole kwa msiba wa kumpoteza kaka,” ameeleza Dk. Biteko.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewashukuru Watanzania kwa kumfariji katika kipindi hichi cha msiba wa kaka yake.

Amesema amepokea salamu za pole kutoka kwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar, Dk.Hussein Ali Mwinyi na watanzania wote wanaompa pole na kumfariji.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here