Home KITAIFA MAJALIWA: NMB ENDELEENI KUTOA MIKOPO KWA WAFANYABIASHARA WANAOJIKITA KATIKA SEKTA YA GESI

MAJALIWA: NMB ENDELEENI KUTOA MIKOPO KWA WAFANYABIASHARA WANAOJIKITA KATIKA SEKTA YA GESI

Google search engine
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (wapili kushoto)akimsikiliza Meneja wa NMB Kanda ya Kusini, Faraja Ng’ingo, kabla ya kuzindua Mkutano Mkuu wa Saba wa Jukwaa la Wahariri (TEF) unaofanyika mjini Lindi. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack. NMB ilishiriki kama mdhamini wa Mkutano Mkuu huo.

Na MWANDISHI WETU

LINDI

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ameishauri Benki ya NMB Kanda ya Kusini kuendelea kutoa huduma ya mikopo kwa wajasirimali na wafanyabiashara wa kati  waliojikita katika sekta ya gesi na mafuta.

Majaliwa ameyasema hayo mapema leo Novemba 13, 2023 alipotembelea katika banda la maonyesho la NMB kabla ya kuzindua Mkutano mkuu wa saba (7) wa jukwaa la wahariri (TEF) unaofanyika katika viwanja vya Ilulu Manispaa ya Lindi Mkoani Lindi.

Majaliwa amesema bado wajasiliamali na wafanya biashara wa kati hasa waliopo katika Mikoa ya Lindi na Mtwara ambao wanahusika kwa karibu na miradi ya sekta ya Gesi kuhamasishwa kuwekeza katika sekta hiyo ambapo pamoja na mambo mengine mikopo hiyo itawavutia kuendelea kuwekeza .

” Endeleeni kuwawezesha wajasilimali waliojiwekeza katika sekta hii ya gesi na hata wale wafanyabiashara wa kati ili hawa wote wawe katika guludumu lenu wahusike na hasa hawa katika Mikoa hii ambayo inahitaji hamasa na muendelee kulitamka ili watu waingie ikiwa ni maandalizi ya kupokeaji wa Mradi wa gesi asilia wa LNG 

Kwa upande wake Meneja wa NMB Kanda ya kusini Faraja Ng’ingo amesema Katika kusaidia sekta hiyo ya mafuta na uchumi  wa  Gesi   Benki ya NMB inajivunia kuwa na rasilimali zenye thamani ya takribani TZS 11.5 trilioni pamoja na amana zipatazo TZS 8.2.trilioni,  ambapo uwezo wao ni kitoa mpaka bilioni 420 kwa mteja mmoja 

 “Kama ujuavyo, Sekta ya Mafuta na Gesi  ipo kwenye hatua ya ukuaji mkubwa ambao sisi kama Benki, tumeamua kuingia kwa nguvu moja kuhakikisha sekta hii inakua na kuchochea shughuli za utaftaji  Mafuta na Gesi  na hivyo kusaidia ongezeko la mapato ya serikali ya Tanzania kupitia Mrabaha au tozo za ukaguzi na ushuru wa huduma, 

“Benki hutoa huduma ya Asset Financing ambayo Ni mikopo nafuu ya vifaa Mahususi Kwa Sekta Binafsi Ya Mafuta na Gesi  ambapo tunatoa Mikopo kadri ya mahitaji yao, kwa ajili ya kupanua na kuboresha huduma. ” alieleza Ng’ingo 

Ngingo aliongeza kuwa  mpaka Septemba 2023, tumeshatoa mikopo yenye thamani ya $330 mln takriban Shilingi Bilioni 842 kwa wadau wa Mafuta na Gesi  wadogo, wakati na wateja wakubwa. Lengo letu likiwa kuwa fikia wateja wengi zaidi wenye vigezo na uhitaji ilikuimarisha sekta ya Mafuta na Gesi  na kukuza uchumi wa nchi.

“Tuna imani wadau wa Mafuta na Gesi wa hapa Lindi wataendelea kuchangamkia fursa hizii na hivyo kuona sekta yetu ya Mafuta na Gesi  inakua kwa ufanisi ziadi.

Zaidi ya hapo, pia tunategemea kupitia mkutano huu, tutapata mrejesho na mawazo mbalimbali kutoka Jukwa la Wahariri juu ya huduma zetu. Mawazo yatakayotusaidia kuendelea kufanya maboresho ya huduma na suluhishi mbalimbali za kibenki.” Alisema Ng’ingo .

“Kwa juhudi hizi endelevu, Benki ya NMB imeona ni muhimu kuwa moja ya wadhamini kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa TEF ambao pia utajadili fursa za sekta ya gesi na mafuta hususan hapa Lindi na kuwapa maendeleo ya benki yao pamoja na huduma mbalimbali ambazo zinatolewa ili kuwapa uelewa zaidi wa huduma na masuluhisho za kifedha zilizopo.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here