Na MWANDISHI WETU
-ARUSHA
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Samia Suluhu Hassan amewatunuku kamisheni maafisa wanafunzi 575 wa kundi la 04/20-Shahada ya sayansi ya kijeshi (BMS) na kundi la 70/20-Regular katika cheo cha Luteni Usu .
Rais Samia amewatunuku kamisheni maafisa hao katika chuo cha kijeshi Monduli ambapo kati yao Wanaume ni 482 na wanawake wakiwa ni 98.
Aidha maofisa wanafunzi hao wamekuwa Maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambapo maofisa wapya kundi 04/20 BMS ni 62 ambao wamepata mafunzo katika chuo hicho.
Alisema kuwa kundi la 70/20-Regular ina idadi ya 447 wamepata mafunzo yao kwa muda wa mwaka mmoja ambapo miongoni mwao maafisa wanafunzi ni 66 ambao wamepata mafunzo ya Urubani kutoka nchi Rafiki.
Awali kabla ya kutunuku kamisheni Rais Samia alikagua gwaride lililoandaliwa na maafisa wanafunzi kutokana na maelekezo ya Mkuu wa Chuo cha mafunzo ya kijeshi Monduli Brigedia Jenerali Jackson Jairos Mwaseba na kusimamiwa na mkufunzi Mkuu Kanali Nilinda William Duguza .
Ambapo zawadi zilitolewa kwa maafisa wanafunzi waliofanya vizuri zaidi kwa makundi yote mawili na kumvisha bawa afisa Mwanafunzi Rubani kwa niaba ya Marubani wenzake.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha mafunzo ya kijeshi Brigedia Jenerali Jackson Jairos Mwaseba amesema Chuo kinaona fahari kubwa kwani hii ni mara ya kwanza kuwezesha mafunzo ya shahada hiyo kwa kujisimamia pasipo na ushirikiano wa mafunzo wa Chuo cha uhasibu Arusha (IAA)
Hata hivyo sherehe hizo zimezinduliwa na viongozi mbalimbali wa Serikali ikiwemo Mkuu wa majeshi ya ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda,Mnadhimu Mkuu JWTZ Luteni Jenerali Salum Haji Othman,makamanda mbalimbali,Majenerali wastaafu wa JWTZ,Wawakilishi wa nchi Rafiki.