*UCSAF yaeleza mkakati madhubuti, mradi wa tiba mtandao mbioni kufungwa hospitali zote nchini
Na MWANDISHI WETU
-BEST MEDIA, DAR ES SALAAM
SASA ni kicheko kila kona. Ndivyo unaweza kusema hasa kutokana na mkakati wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), kuwa mbioni kufunga mtandao wa inteneti katika vituo vyote vya mabasi ya Mwendokasi mkoani Dar es Salaam.
Ni wazi hatua hiyo inakwenda kuleta mapinduzi ya kijitali nchini na kuwafanya wananchi kuwa kwenye ulimwengu wa kisasa.
Akizungumza na Wahariri wa vyombo vya habari nchini katika kikao kazi kilichoitishwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Justina Mashiba, amesema kuwa kwa sasa wapo katika hatua za manunuzi ili kukamilisha mradi ambao wanaufanya kwa kushirikiana na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (DART).
“Utekelezaji wa mradi huu (ufungaji wa Inteneti katika vituo vya mabasi ya Mwendikasi) uko hatua za awali za manunuzi, hivyo lengo letu ni kuleta mapinduzi ya kweli kwenye sekta ya mawasiliano nchini, ambapo mtandao wa intaneti katika vituo vya magari ya Mwendokasi (DART PHASE 1 & 2)
“Tunataka mtu akiwa kituoni awe na uwezo wa kupata intaneti pasi na shaka kama njia sahihi ya kuleta mapinduzi ya uchumi wa kidigitali,” amesema Mashiba
MRADI WA TIBA MTANDAO
Mashiba, amesema kuwa UCSAF inatekeleza radi huu kwa kushirikiana na DIT, MNH, MOI na Hospitali zingine Hospitali zilizounganishwa Morogoro RRH na zinazokamilishwa ni pamoja na Ruvuma, Tanga, Katavi, Nzega na Chato.
“Kwa upande wa Zanzibar tunaunganisha Hospitali ya Abdalla Mzee iliyopo Pemba na Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja iliyopo Unguja ambapo utekelezaji wake upo katika hatua za mwisho,” amesema Mashiba
UJENZI WA MINARA VIJIJINI
Afisa Mtendai Mkuu huyo wa UCSAF, amesema kuwa taasisi yao imeingia mikataba na watoa Huduma ya Mawasiliano (Makampuni ya simu) kufikisha Huduma ya Mawasiliano katika kata 1974 zenye vijiji 5,111 kwa kujenga jumla ya minara 2,149, ambapo minara yote hii ikikamilika wananchi takriban 23,798,848 watapata Huduma hiyo ya Mawasiliano ya simu kwa uhakika.
“Mpaka sasa, jumla ya kata 1,197 zenye vijiji 3,613 na wakazi takribani 14,572,644 wameshafikishiwa Huduma ya Mawasiliano kwa jumla ya minara 1,321 iliyojengwa tayari katika kata hizo.
“Utekelezaji unaendelea katika 777 yenye minara 828, vijiji1,498 na wakazi 9,226,204 Gharama (Ruzuku) za utekelezaji wa mradi huu ni takriban Shilingi bilioni 326,” amesema
MRADI WA TANZANIA YA KIDIGITALI
Mashiba, amesema kuwa jumla ya Minara 758 itajengwa katika kata 713 na mikoa 26 itanufaika katika wilaya 127 zitanufaika pindi mradi huu utakapokamilika
“Jumla ya wakazi milioni 8.5 watanufaika na mradi, Airtel atajenga minara 169, TTCL minara 104, Honora Minara 261, Halotel minara 34 na Vodacom minara 190.
“Kazi zilizofanyika jumla ya Shilingi bilioni 32.9 zimekwisha lipwa kwa watoa huduma na UCSAF kama Advance, Payment kwa watoa huduma wote kupitia ruzuku ya DTP, kiasi cha Shilingi billioni 12.96 zimelipwa kwa Vodacom na Airtel,” amesema Mashiba
Pamoja na hali hiyo amesema kuwa vibali vya mazingira (Provisional Environmental Certificate) zimetolewa kwa minara yote 758 ambapo watoa Huduma wanaendelea kufanya tathmini ya maeneo ya kujenga minara.
Amesema kuwa Halotel ameanza ujenzi ambapo amesimamisha minara mitano tayari imeanza kazi.
HALI YA MAWASILIANO NCHINI
Kutokana na kukua kwa sekta ya mawasiliano nchini UCSAF imeendelea kuimarisha hali hiyo katika maeneo mbalimbali ikiwamo katika sekta ya kilimo huku jumla ya shule 1120 zimefikishiwa Vifaa vya TEHAMA
Mashiba, amesema kuwa kwa wastani shule hupewa Kompyuta tano, Printa moja na Projekta moja.
“Kwa mwaka wa fedha 2022/23, Shule 150 zilifikishiwa vifaa vya TEHAMA Bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/23 ni Shilingi 1,876,900,000.
“Mradi wa kupeleka vifaa maalum vya kujifunzia kwa shule zenye watoto wenye mahitaji maalum, ambapo shule nane zimefikishiwa vifaa vya TEHAMA ambapo vifaa hivyo ni pamoja na TV, Braille Machine (Nukta Nundu) Orbit reader (Machine za Kisasa), Laptops, Embosser (Printa ya nukta nundu).
“Shule hizo zitakazonufaika ni pamoja na Shule ya Sekondari ya Mpwapwa (Mpwapwa-Dodoma), Sekondari ya Mkolani (Mwanza), Sekondari ya Kashaulili (Mpanda-Katavi), Sekondari ya Morogoro (Morogoro), Sekondari ya Shinyanga (Kishapu-Shinyanga), Sekondari ya Wavulana Songea (Songea), Sekondari ya Kazima (Tabora) na Sekondari ya Haile Selassie (Mjini Magharibi) kwa gharama ya Shilingi milioni 575,000,000,” amesema Mashiba
MTANDAO WA INTANETI MAENEO YA WAZI
Afisa Mtendaji Mkuu huyo, amesema kuwa maeneo sita yamenufaika na mradi Chuo cha Maendeleo ya Jamii cha Lungemba (Mafinga), Nyerere Square (Dodoma), Ndaki ya Habari na Elimu Angavu (CIVE, UDOM), Soko la Tabora (Tabora), Kiembe Samaki (Unguja) na Soko la Buhongwa (Mwanza).
Amesema kuwa mradi huo umekamilika katika vituo vyote sita yamefungwa mtandao wa intaneti katika maeneo ya wazi kwa gharama ya Shilingi 174,000,000
MTANDAO WA INTANETI VIWANJA VYA SABASABA
Mashiba, amesema kuwa pamoja na kuwa na mikakati kadhaa lakini bado UCSAF inapeleka intaneti katika maeneo 17 ndani ya viwanja vya Sabasaba ambao nao ni wanufaika wa mradi huo.
Ameyataja maeneo hayo ambayo ni Main Gate Mizigo Gate, Msomali Gate, Sabasaba Hall, DART Gate, Wasanii Area, Windoek, Wizara ya Fedha, TEHAMA Pavilion, Dom Hall, Food Area, Karume Hall, Kizota Gate (Inside), Kobil Gate, Magereza Gate, Wizara ya Viwand ana Kilimanjaro Hall ambapo gharama iliyotumika katika mradi ni Shilingi milioni 200.
UJENZI WA VITUO VYA TEHAMA ZANZIBAR
Amesema vituo 11 vimejengwa Zanzibar, Pemba vinne na Unguja Saba, vituo vinasaidia kutoa mafunzo ya TEHAMA, kituo cha mwisho ni kilichojengwa BWEFUM ZANZIBAR na kuzinduliwa na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi ambacho kilizinduliwa Oktoba 26, 2022 ambapo kituo kimejengwa kwa gharama ya Shilingi 147,000,000.
“Vituo hivyo ni pamoja na Tunguu, Mwera, Kitogani, Mkokotoni, Kiembe Samaki, Mahonda, Wete, Machomanne, Micheweni, Jonza na Bwefumu,” amesema Mashiba
VITUO VYA TEHAMA KWA KUSHIRIKIANA NA TPC
Amesema kuwa vituo 11 vimeanzishwa kwa kushirikiana na Shirika la Posta Tanzania (TPC) ambapo UCSAF ilitoa kompyuta pamoja na Printa.
UBORESHAJI HUDUMA ZA UTANGAZAJI
Kutokana na hali hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu huyo wa UCSAF amesema kuwa baada ya upembuzi wa kitaalamu, maeneo sita yalibainika kuwa na uhitaji wa kujengewa vituo vya kurushia matangazo ya redio ambayo ni Halmshauri ya Wilaya ya Kasulu, Same, Kilindi, Mbulu, Kondoa na Rufiji.
“UCSAF itajenga mnara mmoja kwa kila Halmashauri kwa ajili ya Community Radio, mkataba kwa maeneo haya sita tayari umesainiwa. Ujenzi unaendelea katika maeneo matano (Same, Kilindi,Kasulu, Kondoa DC na Mbulu), ambapo halmashauri ya Wilaya ya Rufiji wanasubiri kukamilika kwa barabara ya kupelekea vifaa eneo la mradi.
“Kwa Mwaka wa fedha 2022/23, Wilaya ya Arusha DC, Mpimbwe (Katavi), Bariadi (Simiyu), Biharamulo (Kagera) zimenufaika na hatua za awali za utekelezaji wa mradi zinaendelea.
“UCSAF inashirikiana na TBC kuboresha usikivu wa matangazo yake jumla ya vituo 16 kujengwa, ambapo utekelezaji wa miradi katika maeneo kumi na sita n kati ya hayo 11 umekamilika. Maeneo hayo ni Kisaki mkoani Morogoro, Mlimba mkoani Morogoro, Ludewa mkoani Njombe, Makete mkoani Njombe, Ruangwa mkoani Lindi, Ngara mkoani Kagera, Mlele mkoani Katavi, Kyela mkoani Mbeya, Uvinza mkoani Kigoma, Ngorongoro mkoani Arusha na Mbinga mkoani Ruvuma,” amesema
Aidha, amesema utekelezaji wa miradi unaendelea katika Matano ya Lushoto-Mkinga mkoani Tanga, Kyerwa mkoani Kagera, Chemba mkoani Dodoma, Kiteto mkoani Manyara na Chunya mkoani Mbeya Kazi zinajumuisha Ujenzi wa vituo vya kurushia matangazo ya redio ikiwemo mnara, vyumba vya mitambo, miundombinu ya nishati ya umeme, chumba cha mlinzi na choo na kiasi cha ruzuku iliyotumika ni shilingi bilioni 4.5
Kwa mwaka wa Fedha 2023/24 maeneo yatakayonufaika ni pamoja na Rombo, Usangi na Geita, ambapo gharama yake ni bilioni 1,350,000,000
MRADI WA KUONGEZA UWEZO WA MINARA
Mashiba, amesema kuwa UCSAF imeingia makubaliano na watoa huduma kuongeza nguvu minara 127, mradi huu umekamilika.
“Kupitia mradi wa DTP, Mei 13, 2023 watoa huduma (Makampuni ya simu) yaliingia makubaliano na Serikali ambapo jumla ya minara 304 itaongezewa nguvu. Mpaka kufikia Novemba 20, 2023, Jumla ya minara 111 tayari imeshaongezewa nguvu kutoka kwa watoa huduma.
“(Vodacom-30, Airtel-25 na Honora-56) hharama za mradi huu ni TZS 5,149,164,696. Utekelezaji wa maeneo yaliyobakiwa yanatarajiwa kumalizika ifikapo Disemba 2023,” amesema
MRADI WA MAFUNZO KWA WALIMU
Amesema kuwa mafunzo yameanza 2016 Walimu wamepatiwa mafunzo 3,465 Walimu kutoka Tanzania Bara Walimu kutoka Tanzania Visiwani 3,139, 326
Mwaka wa Fedha 2023/24 kutoka Songwe Tabora Walimu watapatiwa mafunzo kwa ufadhili wa UNICEF 42 mafunzo haya yanatarajiwa kugharimu Shilingi milioni 50,000,000.
KUTOA VIFAA VYA TEHAMA
Amesema UCSAF imepanga kutoa vifaa 250 vya TEHAMA kwa ajili ya kuboresha utoaji wa huVduma za posta.
“UCSAF inatekeleza mradi huu kwa kushirikiana na Shirika la Posta Tanzania (TPC). Hatua za manunuzi zimekamilika na mkataba umeshasainiwa na mzabuni kwa ajili ya kuleta vifaa hivi,” amesema
SIKU YA WASICHANA NA TEHAMA
Zaidi ya wasichana 954 wamepata mafunzo ya TEHAMA tangu kuanzishwa kwake mwaka 2016.
Kwa Mwaka wa fedha 2023/24, Wasichana 110 watafanyiwa mafunzo katika mikoa ya Songwe-30, Tabora-40 na Kigoma-40 kwa kushirikiana na UNICEF, ambapo katika mradi huu UNICEF wametoa bajeti ya Shilingi 90,000,000.