*Wateja Airtel kuunganishwa na GB 75 kwa miezi 12 wakinunua simu ya Airtel katika maduka ya Airtel na itel popote nchini
*Ni toleo maalum kwa ajili ya msimu huu wa Sikukuu
Na MWANDISHI WETU
-DAR ES SALAAM
KAMPUNI ya Simu za mkononi ya Airtel Tanzania na kampuni ya kutengeneza simu ya itel kwa pamoja wameshirikiana wamezindua simu mpya ya itel A70 iliyoambatanishwa na ofa ya bando ya intaneti yenye kifurushi cha Bure cha GB 75 ambacho kinadumu kwa muda wa miezi kumi 12.
Ushirikiano wa Airtel na itel unawahakikishia Watanzania uwezo wa kupata simu za kisasa za smartphone zenye ubora wa juu kwa gharama nafuu zaidi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Novemba 23, 2023, wakati wa uzinduzi wa simu hiyo ya kisasa kabisa yenye ofa kabambe, Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania, Beatrice Singano amesema “Tunajivunia ushirikiano wa Airtel na itel kwa kuzindua simu mpya na ya kisasa ya A70.
“Wenzetu wa itel wanalenga kuhudumia wateja wa kipato cha kati na cha chini kwa bidhaa zenye ubora na unafuu, hivyo basi Airtel ikiwa moja ya makampuni yanayotoa huduma za smartphone za kisasa na uhakika, tukaona tuwafikishie ofa hii kabambe watanzania wote ili kuwawezesha kuendana na ulimwengu wa kidigitali kwa kutumia mtandao wetu ulio bora na ulioenea kote nchini na simu ya itel,” amesema Singano
Amesema Simu ya A70 itakuwa inapatikana kwenye maduka yote ya Airtel na itel kote nchini ikiwa na ofa ya kifurushi cha bando ya intaneti ya 75GB kwa muda wa miezi 12.
Kwa upande wake, Meneja wa Chapa wa itel kutoka itel Mobile, Thomas Wang, amesema kuwa ni furaha kubwa sana kushirikiana na Airtel kuzindua simu mpya ya kisasa ya itel A70 ambayo ni Smartphone ambayo ni toleo la kisasa na inapatikana kwa bei nafuu kabisa Tanzania nzima.
Simu ya A70 ni nyepesi sana na inatoa suluhisho bora kwa watumiaji wa huduma za kidigitali kwa uhakika na haraka kabisa itapatikana kwa gharama nafuu,
Ameongeza kuwa simu ya itel A70 ina uwezo wa 128GG ROM + 8GB RAM, 6,6” na ukubwa wa kioo wa 13MP super HDR CAM. Hivi vyote kwa pamoja vinampa mtumiaji kufarahi matumizi ya simu hii pamoja na kumpa Uhuru wa mawasiliano.
“Sababu kubwa ya ushirikiano baina ya Airtel na itel ni kuwapa Watanzania kuwa na uwezo wa kutumia smartphone za kisasa zenye ubunifu wa hali ya juu kwa gharama nafuu pamoja na kufurahi kifurushi cha intaneti cha 75GB kutoka Airtel kwa mwaka mzima,” amesema Wang