Home KITAIFA Wateja 100 wajizolea Milioni 10/- za Droo ya 3 ‘NMB MastaBata Halipoi’

Wateja 100 wajizolea Milioni 10/- za Droo ya 3 ‘NMB MastaBata Halipoi’

Google search engine
Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Tegeta, Peter Msaki (katikati), akibonyeza kitufe cha kompyuta kuwatafuta washindi wa droo ya tatu ya Kampeni ya NMB MastaBata Halipoi iliyofanyika katika tawi hilo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja wa Kituo cha Kadi Benki ya NMB, Sophia Mwamwitwa na kushoto ni Afisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Pendo Mfuru. (Na Mpiga Picha Wetu).
Meneja wa Kituo cha Kadi Benki ya NMB, Sophia Mwamwitwa, akizungumza na mmoja kati ya washindi 100 wa droo ya tatu ya Kampeni ya NMB MastaBata Halipoi iliyofanyika katika Tawi la Tegeta jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Pendo Mfuru na katikati ni Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Tegeta, Peter Msaki. (Na Mpiga Picha Wetu).

NA MWANDISHI WETU

DROO ya tatu ya Msimu wa Tano wa Promosheni ya kuhamasisha matumizi yasiyohusisha pesa taslimu inayoendeshwa na Benki ya NMB, ijulikanayo kama ‘NMB MastaBata Halipoi,’ imefanyika jijini Dar es Salaam Alhamisi ya Novemba 23, ambako washini 100 wamejinyakulia zawadi ya pesa kiasi cha Sh. Milioni 10 (sawa na Sh. 100,000 kila mmoja).

MastaBata Halipoi iliyozinduliwa Oktoba 27 mwaka huu, ni maalum kwa wateja wa NMB wenye MasterCard wanaozitumia kufanya malipo katika Vituo vya Mauzo (POS), wanaotumia MasterCard QR za benki hiyo, pamoja na huduma za malipo ya kimtandao ‘e-commerce,’ ambapo washindi hao 100 wanafanya idadi ya wanufaika wake kufikia 300 walioshinda Sh. Mil. 30.

Droo ya tatu imefanyika katika Tawi la NMB Tegeta, ambako Meneja wa tawi hilo, Peter Msaki, aliwataka wateja wa benki yake kudumisha utamaduni wa matumizi kwa njia ya kadi, ili kujiwekea nafasi kubwa zaidi ya kuingia katika kinyang’anyiro hicho na kushinda zawadi zenye thamani ya zaidi ya Sh. Milioni 350 zitazoenda kwa washindi 1,492.

“Tuko hapa kutafuta na kuwatangaza washindi 100 wa wiki ya tatu wa kampeni hii, ambao kila mmoja atajisjhindia Sh. 100,000, tayari tumeshatoa zawadi kwa washindi 200 wa wiki mbili za kwanza za kampeni hii, ambayo itafikia ukomo baada ya miezi mitatu tangu Oktoba 27 ilipozinduliwa.

“Hii ina maana kwamba kwa wiki 12 za miezi mitatu, tutatoa jumla ya Sh. Mil. 120 kwa wateja 1,200 – yaani 100 kila wiki, huku wateja 240 wa papo kwa papo, yaani 20 kila wiki wakijinyakulia Sh. Milioni 1 na washindi 10 wa droo za mwezi (wateja watano kila mwezi), wakitarajiwa kugharamiwa ziara ya kwenda Kendwa Rocks Zanzibar na ‘pocket money’ ya Sh. 200,000 kila mmoja.

“Kama hiyo haitoshi, MastaBata Halipoi, itawazawadia washindi 30 (sawa na washindi 15 kila mwezi) jumla ya Sh. Mil. 15, yaani sawa na Sh. 500,000 kila mmoja na hitimisho litalofanyika katika mwisho wa mwezi wa tatu ‘Grand Finale’, itashuhudiwa wateja 12 na wenza wao wakifanya ziara ya siku tano nchini Afrika Kusini iliyogharamiwa kila kitu na NMB,” alibainisha Msaki.

Meneja huyo aliwataka wateja wa benki yake kuendelea kufanya malipo ya manunuzi yao kwa njia ya kadi, ambayo ni rahisi, nafuu na salama zaidi, ili kujishindia zawadi mbalimbali zilizotengwa katika msimu huu, unaoambatana na Sikukuu za Krismasi (Desemba 25), Boxing Day (Desemba 26) na mwaka mpya Januari 1, 2024.

Droo hiyo ilifanyika chini ya usimamizi wa Ofisa wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Pendo Mfuru, ambaye aliwahakikishia wateja wa NMB, kwamba bodi yake ambayo ina mamlaka kisheria ya kuratibu na kusimamia michezo ya kubahatisha nchini, imeridhishwa na mifumo ya kisheria inayofanywa na benki hiyo katika kupata washindi.

“Niko hapa kwa niaba ya GBT, bodi ambayo kisheria ndio yenye mamlaka juu ya michezo hii. Naipongeza NMB kwa kufuata vigezo na masharti wanapoendesha droo zao na niwahakikishie wateja wao kwamba, hakuna ukiukwaji wowote wa kanuni na sheria, hivyo wawe huru kushiriki na kila mwenye bahati ataibuka na zawadi yake bila wasiwasi,” alisisitiza Pendo.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here