Home KITAIFA BENKI YA NMB MLIPA KODI MKUBWA NA BORA ZAIDI TANZANIA MWAKA 2023

BENKI YA NMB MLIPA KODI MKUBWA NA BORA ZAIDI TANZANIA MWAKA 2023

Google search engine
Naibu waziri Mkuu na waziri wa Nishati, Dotto Biteko akimkabidhi Tuzo ya mlipa kodi bora Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya NMB, Ruth Zaipuna katika hafla ya tuzo za TRA zilizofanyika mwishoni mwa wiki iliyo pita jijini Dar es Salaam, Benki ya NMB imeibuka Mshindi wa jumla katika tuzo hizo. Na kushoto ni Afisa Mkuu wa Rasilimali watu wa Benki ya NMB, Emmanuel Akonaay.

Na MWANDISHI WETU

-DAR ES SALAAM

NOVEMBA 24, 2023 ilikuwa ni siku ya Mlipa Kodi 2023, Benki ya NMB iliibuka Mshindi wa Jumla Kitaifa, kama Mlipa Kodi Mkubwa Zaidi Tanzania na kama Mlipa Kodi Bora Zaidi anayelipa Kodi kwa hiari (Most Compliant Tax Payer).

Huu ni mwaka wa pili mfululizo kwa Benki ya NMB kupata tuzo hizi.

Jumla ya Tuzo ilizopata Benki ya NMB ni: Mshindi wa Jumla Kitaifa: Taasisi inayolipa Kodi kubwa zaidi nchini Tanzania (Sekta zote),  Mshindi wa Jumla Kitaifa: Taasisi Bora inayolipa Kodi kwa hiari kwa  kuzingatia misingi na kanuni bora za ulipaji kodi (Most Compliant Tax Payer), Mshindi wa Kwanza: Mlipa Kodi mkubwa zaidi katika kundi la Taasisi za Fedha nchini Tanzania (mara ya tatu mfululizo).

Akiongea mara baada ya kupokea Tuzo hizo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Bi. Ruth Zaipuna alisema Tuzo hizo ni matokeo chanya ya Misingi Imara ya Utawala Bora na Uadilifu, kuzingatia kanuni za ulipaji kodi, ufanisi katika kuendesha biashara na ubunifu wa suluhishi bora za kifedha kwa wateja.

“Nawashukuru wateja wetu na Watanzania wote kwa kuendelea  kuiamini Benki ya NMB kama mshirika wao kwenye biashara na shughuli zao, naishukuru Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuweka mazingira wezeshi ya kufanya Biashara nchini na kipekee nawashukuru wafanyakazi wenzangu wote wa Benki ya NMB kwa kuendelea kufanya kazi kwa ari, bidii na kwa Uzalendo mkubwa kwa maslahi mapana ya Benki na nchi yetu kwa Ujumla.

Tuzo hizo za Mamlaka ya Mapato Tanzania zimetolewa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Dotto Biteko katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Kama mdau wa maendeleo, Benki ya NMB tutaendelea kuendesha biashara yetu kwa kuzingatia sheria na kanuni za nchi ili kuendelea kuchangia kikamilifu ujenzi wa uchumi wa Taifa letu.

Tuzo hizo za kuwatambua walipa kodi bora wa mwaka wa fedha wa 2022/23 zilitolewa na Naibu Waziri Mkuu, Dk. Dotto Biteko, aliyesisitiza azma ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kuendeleza mageuzi ya kuboresha mazingira ya kufanya biashara nchini.

Ajenda hiyo alisema ni muhimu kuzidi kuwavutia wawekezaji ili kupanua wigo wa vyanzo vya mapato na ulipaji kodi wa hiari kwa ajili ya kupata mapato ya kuliendeleza taifa.

“Kuwatunuku walipa kodi ni suala muhimu kutokana na mchango wao katika maendeleo kwani bila wao rasilimali zinazohitajika kuchangia ukuaji wa uchumi haziwezi kupatikana kikamilifu,” Dk. Biteko alibainisha.

“Hawa ni wadau wakubwa katika ujenzi wa taifa ambao hawapaswi kukwazwa kwa namna yoyote ile bali kuelimishwa zaidi na kuhudumiwa vizuri katika ulipaji kodi wao na Serikali hii inalizingatia hilo kwa karibu sana.”

Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande, aliipongeza TRA kwa kuziendeleza tuzo hizo ilizozianzisha mwaka 2006 akisema kutambua mchango wa walipa kodi kunasaidia mamlaka hiyo kutimiza malengo ya  ukusanyaji mapato.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here