Home BIASHARA NMB yaunga Benki 17 kwenye mtandao wake wa ATM nchini

NMB yaunga Benki 17 kwenye mtandao wake wa ATM nchini

Google search engine
Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande (kulia) , akifurahi baada ya kuzindua rasmi ushirikiano wa Benki ya NMB na UBX inayounganisha benki 17 kwenye mtandao wake wa Umoja Switch ambao umeiwezesha Benki ya NMB kuunganisha benki hizo kwenye mtandao wake wa mashine za kutolea fedha. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna na katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya UBX, SabaSaba Moshingi

Na MWANDISHI WETU

-BST MEDIA, DAR

USHIRIKIANO wa Benki ya NMB na UBX inayounganisha benki 17 kwenye mtandao wake wa Umoja Switch umeiwezesha Benki ya NMB kuunganisha benki hizo kwenye mtandao wake wa mashine za kutolea fedha (yaani ATM interoperability).

Ushirikiano huo unalenga kuongeza wigo wa upatikanaji wa mashine za ATMs na kupunguza gharama za miamala ya ATM kwa wateja wa benki hizo na watanzania kwa ujumla.

Kupitia ushirikiano huu wa Benki ya NMB na UBX, Watanzania watanufaika na mambo kahaa ikiwamo upatikanaji wa huduma za ATM  ambapo wateja benki zote 17 za Umoja Switch na wateja wa Benki ya NMB watakuwa na uwezo wa kufanya miamala na kupata huduma za kibenki wakati wowote kupitia mtandao wa ATMs zaidi ya 700 za NMB zinazopatikana nchi nzima na ATMs za Umoja Switch (zaidi ya 280) na hivyo kuongeza wigo wa upatikanaji wa huduma.

Pi unafuu wa gharama kwa wateja ambapo ushirikiano huo unaongeza ufanisi na kuleta unafuu mkubwa wa gharama za miamala ya ATM.

Mbali na hilo pia gharama za miamala ya ATM kwa wateja wa benki hizo 17 waliokuwa wanatumia ATM za NMB na wateja wa NMB waliokuwa wanatumia ATM za benki hizi zinaenda kupungua kwa zaidi ya asilimia 70.

Pia ujumuishwaji wa Kifedha unatajwa kama chachu kwenye ushirikiano huo unaotajwa kuongeza matumizi ya kadi kwenye ATM nchini na kupunguza foleni matawin wani hatua hiyo ni njia mbadala ya kuongeza ujumuishaji rasmi wa kifedha nchini.

Ufanisi wa Mabenki benki shiriki zitaweza kufikia maeneo yaliyo mbali na ambayo hapo awali ilikuwa vigumu kwa taasisi moja kuyafikia kwa kuweka ATM.

Hatua hii inatajwa ni tukio la kwanza kuwa na makubaliano ya namna hiyo kufanyika na hivyo makubaliano haya yanaandika historia mpya katika sekta ya kifedha nchini Tanzania

Akizungumza kwenye hafla hiyo Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna amesema kuwa “Nina Imani ya kuwa ushirikiano huu utakuwa mwanzo na chachu ya mashirikiano mengine mengi na ya kimkakati katika sekta yetu ya kibenki nchini Tanzania kwa manufaa ya wateja wetu na Watanzania kwa ujumla.

“Kupitia mashirikiano ya kimkakati kama haya tutaweza kupiga hatua zaidi katika utoaji wa huduma nafuu, rahisi na salama za kibenki kwa watanzania wote, na hivyo kuchochea ukuaji wa kiuchumi wa mtanzania mmoja mmoja na taifa letu kwa ujumla,” amesema Zaipuna

Kwa upande wake mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi huo Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande aliipongeza Benki ya NMB na UBX na kushauri ushirikiano huo uendelee kwa manufaa ya nchi.

Hafla hii ilihudhuriwa pia na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya UBX, SabaSaba Moshingi na viongozi kutoka mabenki mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na viongozi wa Benki 17 zilizo chini ya Umoja Switch.

Benki zilizo chini ya Umoja Switch ni pamoja na Access Microfinance Bank, Akiba Commercial Bank, Azania Bank, Bank of Africa, DCB Commercial Bank, Letshego Bank, Maendeleo Bank na Mkombozi Commercial Bank.

Zingine ni MUCOBA Bank, Mwalimu Commercial Bank, Mwanga Hakika Bank, Peoples’ Bank of Zanzibar, TCB Bank, Uchumi Commercial Bank, International Commercial Bank na United Bank for Africa.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here