Home KIMATAIFA Elon Musk apoteza taji la mtu tajiri zaidi duniani kwa Jeff Bezos

Elon Musk apoteza taji la mtu tajiri zaidi duniani kwa Jeff Bezos

Google search engine
Elon Musk

Kwa mara ya kwanza baada ya zaidi ya miezi tisa, Elon Musk amevuliwa taji la kuwa mtu tajiri zaidi duniani.

Musk amepoteza nafasi yake katika kipimo cha Mabilionea cha Bloomberg kwa Jeff Bezos baada ya hisa katika kampuni ya Tesla kushuka kwa 7.2% Jumatatu.

Musk sasa ana utajiri wa dola bilioni 197.7 huku utajiri wa Bezos ukiwa dola bilioni 200.3.

Ni mara ya kwanza kwa Bezos, 60, mwanzilishi wa kampuni ya Amazon kushika nafasi ya kwanza ya Bloomberg ya watu tajiri zaidi tangu 2021.

Pengo la utajiri kati ya Musk, 52, na Bezos, ambalo wakati mmoja lilikuwa kubwa kama dola bilioni 142, limekuwa likipungua huku hisa za Amazon na Tesla zikienda pande tofauti.

Ingawa kampuni zote mbili ni kati ya zenye hisa zinazojulikana sana ambazo zimekuza masoko ya hisa ya Marekani, hisa za Amazon zimeongezeka zaidi ya mara mbili tangu mwishoni mwa 2022 na ziko katika rekodi ya juu.

Kampuni ya Tesla iko chini karibu 50% kutoka kilele chake cha 2021.

Hisa za kampuni ya Tesla zilishuka Jumatatu baada ya data ya awali kuonyesha usafirishaji kutoka kwa kiwanda chake huko Shanghai ulipungua hadi chini zaidi katika kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja.

Wakati huo huo, kampuni ya Amazon, imekuwa na ukuaji bora wa mauzo mtandaoni tangu mwanzoni mwa janga la corona.

Siku chache zilizopita Elon Musk alitangazwa kuwa mtu tajiri zaidi duniani, akimpiku mwanzilishi wa Amazon Jeff Bezos.

Utajiri wa mfanyabiashara huyo wa magari ya Tesla na SpaceX umepita dola bilioni 185 sawa na euro 136 bilioni baada ya bei ya hisa za kampuni yake ya magari kupanda.

Lakini je ni nini siri ya ufanisi wake katika biashara? Miaka michache iliopita alizungumzia suala hilo kwa karibu saa moja alipohoijwa na BBC.

  1. Cha msingi sio pesa

Kulingana na mtazamo wa biashara wa Elon Musk – cha msingi sio pesa.

Alipohojiwa mwaka 2014 alisema hajui kiwango cha utajiri wake.

“Sio kwamba kuna rundo la pesa zilizohifadhiwa mahali,” alisema. “Ukweli ni kwamba nina hisa kadhaa katika Tesla, SpaceX, na SolarCity, na katika soko la hisa kila hosa niliyo nayo ina thamani yake.”

Kampuni yake ya magari ya umeme Tesla, imefanya vyema baada ya thamani ya hisa zake kuongezeka hadi zaidi ya dola 700 bilioni katika miaka ya hivi karibuni.

Fedha hizo zinatosha kununua Ford, General Motors, BMW, Volkswagen na Fiat Chrysler, na bado asalie na fedha za kununua gari la Ferrari.

Lakini Musk, ambaye anafikisha umri wa miaka 50 mwaka huu, hatarajii kufariki akiwa tajiri.

Anasema fedha zake zitatumika kujenga majumba katika sayari ya Mars na anasema hatoshangaa kuona utajiri wake wote ukimalizikia katika mradi huo.

Sawa na Bill Gates, huenda akachukulia kama ishara ya kufeli maishani akiwa atasalia na mabilioni kadhaa kwa sababu atakuwa hajatumia fedha hizo kwa njia nzuri.

2. Fuatilia ndoto zako

Ndoto ya kuwa na majumba katika sayari ya Mars ni kidokezo ambacho Elon Musk anaamini ndio ufunguo wa mafanikio.

“Unataka vitu vijavyo maishani kuwa vizuri,” aliambia BBC. “Unataka vitu hivi vipya ambavyo vitafanya maisha kuwa bora.”

Kwa mfano SpaceX. Alisema alibuni kampuni hiyo baada ya kuhisi kwamba mpango wa Marekani wa anga za mbali haukuwa na malengo ya juu zaidi.

“Nilitarajia kuona vitu vya hali ya juu zaidi ambavyo havipatikani duniani vikibuniwa, binadamu kuishi katika sayari ya Mars, kuwa na makao mwezini, na safari za ndege za mara kwa mara kwenda anga za mbali,” alisema.

CHANZO: BBC SWAHILI

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here