Home KITAIFA KINANA AELEZA DHAMIRA YA RAIS SAMIA KUFANIKISHA UCHAGUZI HURU, HAKI

KINANA AELEZA DHAMIRA YA RAIS SAMIA KUFANIKISHA UCHAGUZI HURU, HAKI

Google search engine
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Abdulrahman Kinana akisalimiana na Kiogozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe. katikati Mwanasiacha mahachari toka nchini Kenya Martha Wangari Karua

Na MWANDISHI WETU

-BEST MEDIA, DAR ES SALAAM

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana amewahakikishia Watanzania kuwa Serikali ya CCM inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, imedhamiria kufanya uchaguzi huru na wa haki kuanzia wa serikali za mitaa mwaka huu na uchaguzi mkuu wa 2025.

Hayo ameyasema leo Machi 5, 2024 Jijini Dar es Salaa, alipokuwa akitoa salamu akimwakilisha Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Samia Suluhu Hassan katika Mkutano Mkuu wa Chama cha ACT -Wazalendo.

“Tunakwenda katika uchaguzi wa serikali za mitaa na baadaye mwakani Uchaguzi Mkuu. Kumefanyika mabadiliko ya sheria tatu bungeni. Sheria ya vyama vya siasa, sheria ya tume ya uchaguzi na sheria ya uchaguzi.

“Kuna maoni yametolewa na wadau mbalimbali katika kamati za bunge, bungeni…ukiangalia sheria ile baada ya maoni na ushauri kuna mabadiliko makubwa sana.

“Nataka niwahakikishie kwamba serikali ya Chama Cha Mapinduzi inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, ina dhamira ya dhati katika mwaka huu wa uchaguzi wa serikali za mitaa na mwaka ujao kwenye serikali kuu kuhakikisha kunakuwa na uchaguzi ulio huru na wa haki,” amesema Kinana.

Amesema mbali na kupitisha sheria nzuri ya kuhakikisha kunakuwapo uchaguzi huru na wa haki, pia dhamira ya Rais Dk.Samia kufanikisha hilo inajipambanua katika utekelezaji wake.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here