DAKAR, SENEGAL
SERIKALI nchini Senegal hatimaye imetangaza kuwa itafanya uchaguzi wa rais uliocheleweshwa mnamo Machi 24, 2024
Tangazo hilo limetolewa baada ya kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika Jumatano jioni.
Tangazo hilo limetolewa baada ya kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika Jumatano jioni, ambapo Rais Macky Sall alivunja serikali na kumteua waziri wa mambo ya ndani Sidiki Kaba kuwa waziri mkuu.
Hata hivyo bado kuna mkanganyiko kuhusu tarehe rasmi ya duru ya kwanza ya uchaguzi, baada ya Baraza la juu la Katiba la Senegal, kusema kuwa uchaguzi huo unapaswa kufanyika mwishoni mwa Machi.
Ikiwa uchaguzi huo utaendeshwa mwishoni mwa Machi, utakuwa umefanyika kabla ya mamlaka ya Rais Macky Sall kumalizika Aprili 2, ambayo ilikuwa ni mojawapo ya chanzo kikubwa cha machafuko.
Sall alizua mzozo mbaya zaidi nchini Senegal katika miongo kadhaa kwa kuchelewesha uchaguzi wa urais katika dakika za mwisho, ambao awali ulipangwa kufanyika Februari 25.
Kucheleweshwa kwa kura hiyo kulisababisha maandamano makubwa katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi yenye utulivu, huku wanasiasa wengi wa upinzani na mashirika ya kiraia yakimshuku rais kwa kujaribu kuongeza muda wake madarakani. Hadi sasa hakuna tarehe iliyopangwa ya duru ya pili.
Siku ya Jumatano, Rais Sall alitangaza kwamba Waziri Mkuu Amadou Ba ameandolewa kutoka wadhifa wake ili kuongoza kampeni za urais kwenye kambi yake ya kisiasa.
Mapema wiki, Rais Sall pia aliliomba Baraza la Katiba kutoa maoni yake kuhusu mapendekezo yaliyotokana na “Mazungumzo ya kitaifa” ambayo alikuwa ameyaitisha kujaribu kutafuta mwafaka wa mkwamo wa kisiasa.
Mazungumzo hayo yalipendekeza uchaguzi ufanyike Juni 2 na kwamba Sall asalie madarakani hadi mrithi wake atakapoteuliwa. Lakini Baraza la Katiba la Senegal lilikataa pendekezo hilo.
Katika uamuzi tofauti, Baraza la Katiba pia lilisema kinyang’anyiro cha urais kinapaswa kujumuisha orodha ya wagombea urais 19 ambao tayari wameidhinishwa na chombo hicho.
Wabunge nchini Senegal, hapo Jumatano wamejadili muswada tata wa msamahaunaohusu vitendo vinavyohusishwa na maandamano mabaya katika miaka ya hivi karibuni, wenye lengo la kutuliza mzozo uliosababishwa na kucheleweshwa kwa uchaguzi wa rais nchini humo.
Muswada huo utatoa msamaha kwa waliohusishwa na vitendo vyote vinavyoweza kuorodheshwa kama makosa ya jinai yaliyofanywa kati ya Februari 1, 2021 na Februari 25, 2024, nchini Senegal pamoja na nje ya nchi, yanayohusiana na maandamano au kuwa na misukumo ya kisiasa.Baada ya shinikizo kubwa rais Macky Sall aahidi kuitisha uchaguzi haraka iwezekanavyo
Senegal ilishuhudia matukio kadhaa ya machafuko mabaya kati ya 2021 na 2023, yaliyochochewa haswa na mzozo mkali kati ya kiongozi wa upinzani aliyefungwa sasa Ousmane Sonko na Serikali.
CHANZO: DW