Na MWANDISHI WETU
-DAR ES SALAAM
MTUHUMIWA wa kutapeli na kudhulumu viwanja vya watu na kujimilikisha kinyume na utaratibu jijini Dar es Salaam anayetambulika kwa jina la Paul Mushi leo ametolewa Kituo cha Polisi Oysterbay na kupelekwa Mahakama ya Mwanzo Kinondoni.
Hatua hiyo imekuja baada ya mtuhumiwa huyo kukamwatwa hapo awali kwa tuhuma za kunyang’anya viwanja vya watu kadhaa na sasa amepekwa Mahakamani ili hatua za kisheria ziendelee.
Aidha, mapema jana Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa alitangaza kuanza kwa operesheni maalumu ya kudhibiti matapeli wa ardhi katika Jiji la Dar es salaam.
Operesheni hiyo imekuja siku chache tangu kufanyika kwa Kliniki ya Ardhi ya Jijini Dar es salaam iliyoanza mapema Novemba 2023 na kuhitimishwa mnamo Machi 3, 2024 kwa lengo la kutatua migogoro ya ardhi iliyokuwa inasumbua jiji la Dar es salaam kwa muda mrefu.