Home KITAIFA LIPUMBA: UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA MWAKA HUU HAUNA  TOFAUTI NA MWAKA 2019

LIPUMBA: UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA MWAKA HUU HAUNA  TOFAUTI NA MWAKA 2019

Google search engine

*Ahoji kanuni za uchaguzi kutotolewa hadi sasa, awapa mtihani vijana, Selasini, Mnyika na kiongozi wa ACT Wazalendono nao watupa zigo kwa vijana nchini

Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania(TCD) Profesa Ibrahim Lipumba akizungumza wakati wa kufungua kongamano la Majadiliano rika baina ya Viongozi wa Vyama vya Siasa na Vijana. Majadiliano hayo yamefanyika  leo Machi 11, 2024 katika ukumbi wa Confucious, Chuo kikuu Cha Dar es Salaam.

Na MWANDISHI WETU

-DAR ES SALAAM

MWENYEKITI wa Kituo cha Deokrasia nchini, Profesa Ibrahim Lipumba, aetilia shaka uwazi na haki kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uaotarajiwa kufanyika waka huu pamoja na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Kutokana na hali hiyo amesema kuwa hadi sasa hakuna kanuni za uchaguzi ambazo zinaonyesha picha hali ya uchaguzi huo huku akionyesha wasiwasi wake kwamba hatokuwa na tofauti na ule wa mwaka 2019.

Mkurugenzi Mtendaji Kituo cha Demokrasia Tanzania(TCD) Bernadetha Kafuko akizungumza wakati wa kongamano la Majadiliano rika baina ya Viongozi wa Vyama vya Siasa na Vijana.

Lipumba ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), wakati akifungua kongamano la majadiliano rika baina ya viongozi vijana wa vyama vya siasa leo, Jumatatu Machi 11.2024 Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Jijini Dar es Salaam.

“Nilipoombwa kuwa mgeni rasmi nilipata shida kidogo kujuwa lipi la kuzungumzwa kwa sababu namna mjadala tulivyoupanga ni kana kwamba mazingira yetu ya demokrasia tunaweza kubadilishana mawazo vijana na watu wazima ili tuweze kujifunza katika kuendeleza demokrasia yetu katika nchi yetu.

“Sasa ukiutazama Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ulivyokuwa mwaka 2019 na mpaka hivi sasa hatujui kanuni za uchaguzi huu unaokuja mwaka huu, kwa hiyo naanza kupata wasiwasi kidogo kwamba je, Uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka 2024 utakuwa kama wa 2019 au utakuwa tofauti. Na tunapowahamasisha vijana washiriki wanaenda kushiriki katika mazingira ya namna gani.

“Lakini Uchaguzi wetu Mkuu wa mwaka 2020 ulivyokuwa na tulivyoshiriki, mazingira yalivyokuwepo na kwamba Tanzania Bara vyama vya upinzani vilifanikiwa kupata viti viwili kati ya viti 214 kwa sababu 50 viko Zanzibar, lakini pana mabadiliko ya sheria ambayo yamepitishwa hatujuwi utekelezaji wake ukoje?” amesema na kuhoji Profesa  Lipumba

“Suala sio nani ameshinda ila suala ni kwamba zile kura zinapopigwa yale matokeo, yawe matokeo ambayo kila mmoja anayaamini kwamba haya ni matokeo halali na ni matokeo yanayoonesha matakwa ya wapiga kura” -Prof. Lipumba

Akingumzia suala a ushiriki kwa vijana nchini Profesa Lipumba, amesema kuwa “Ushiriki wa vijana unahitaji vijana wawe wengi kwa maana ukichukua watu wenye umri wa chini ya miaka 18 ni zaidi ya asilimia 59 ya wananchi wote wa Tanzania na ukichukua watu chini ya umri wa miaka 35 ni karibu robo tatu ya wananchi wote wa Tanzania kwa hiyo hii ni nchi ya vijana na siasa lazima ziwe siasa za kutatua matatizo yanayowakabili vijana.

Amesema kuwa isivyo bahati Tanzania ina siasa za kuunga mkono watu na kuunga mkono fedha, sasa ni lazima kuwe na siasa za hoja na sera kwa sababu viongozi hawasimamii watu bali twanasimamia utatuzi wa matatizo yanayoikabili nchi.

Kwa upande wa Balozi wa Marekani hapa nchini, Michael Battle amesema kuwa hakuna mwenye haki zaidi kuliko mwingine na chama kimoja hadi kingine.

“Tanzaniani yenu (vijana), iwe ni Tanzania Bara au Visiwani, ni yenu,” amesema Balozi Battle

Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana, ACT WAZALENDO, Abdul Nondo akiuliza swali katika siasa na namna alivyoingia katika siasa  wakati wa kongamano la Majadiliano rika baina ya Viongozi wa Vyama vya Siasa na Vijana

Akizungumza wakati wa kutoa uzoefu wake, wakati akizungumza na vijana, Mwenyekiti wa Chama cha UDP, John Cheyo amesema kuwa kwenye siasa hakuna pesa wenye pesa ni wezi tu hivyo vijana wawe na wajue kiwa kwenye siasa ni kutatua changamoto za kiuchumi zinazoikabili jamii.

“Siasa iwe Part time tu. Ukiutumia muda huo Full time Maisha ya aweza yasiwe mazuri. Muda mwingi uwe vijana fanyeni kazi za kujipatia kipato halali,” amesema Cheyo.

Joseph Selasini akielezea uzoefu wake katika siasa na namna alivyoingia katika siasa  wakati wa kongamano la Majadiliano rika baina ya Viongozi wa Vyama vya Siasa na Vijana.

Naye Joseph Selasini akitoa uzoefu wake katika siasa amewaasa vija kuwa na wito kweli wa kuongoza na kutatua changamoto.

“Usiingie kwenye siasa kama bendera fuata upepo,” amesema

Kutokana na hali hiyo, Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Doroth Seu amewaasa vijana kutokuwa na haraka ya maendeleo na kupata uongozi.

Katibu Mkuu Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, John Mnyika akielezea uzoefu wake katika siasa na namna alivyoingia katika siasa  wakati wa kongamano la Majadiliano rika baina ya Viongozi wa Vyama vya Siasa na Vijana.

Huku Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika akisema kwamba vijana wanatakiwa kuwa wavumilivu kwenye siasa kwa wananchi kwa sasa wanataka viongozi vijana hivyo wameaswa kuwa na sera ambazo zitakuwa na msaada kwa jamii husika.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here