Home KITAIFA VIONGOZI WAKUU WA LIBYA WAKUBALIANA KUUNDA SERIKALI MPYA

VIONGOZI WAKUU WA LIBYA WAKUBALIANA KUUNDA SERIKALI MPYA

Google search engine
Mkuu wa Baraza la Rais, Mohamed al-Menfi (kushoto) na mbabe wa kivita Khalifa Haftar.Picha: twitter.com/Mohamedelmonfy

Viongozi watatu wakuu nchini Libya wamekubaliana juu ya umuhimu wa kuunda serikali mpya ya umoja ambayo itaratibu uchaguzi uliocheleweshwa kwa muda mrefu.

Viongozi hao ni Mwenyekiti wa Baraza la Rais, Mohamed Menfi, Mwenyekiti wa Baraza Kuu, Mohamed Takala, ambao wote wako mjini Tripoli, pamoja na Spika wa Bunge, Aguila Saleh.

Katika taarifa ya pamoja, viongozi wote watatu wametoa wito kwa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya na jumuiya ya kimataifa kuunga mkono mapendekezo yao.

Miongoni mwa mapendekezo yao ni makubaliano ya kuundwa kwa kamati ya kiufundi itakayotizama vipengele vilivyo na utata.

Viongozi hao walikutana mjini Kairo nchini Misri, kwa mwaliko wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, Ahmed Aboul Gheit.

Mchakato wa kisiasa wa kutatua mzozo wa zaidi ya muongo mmoja nchini Libya umekwama tangu uchaguzi uliopangwa kufanyika Desemba 2021 kushindwa, huku kukiwa na mizozo kuhusu wagombea wakuu wanaostahiki kuwania uchaguzi huo.

CHANZO: DW

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here