Home KITAIFA MAKINDA: WAFANYIENI KAZI MATOKEO YA SENSA

MAKINDA: WAFANYIENI KAZI MATOKEO YA SENSA

Google search engine
Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi, Anne Makinda

Na MWANDISHI WETU

-DAR ES SALAAM

KAMISAA wa Sensa ya Watu na Makazi, Anne Makinda, amewataka watanzania wakiwamo wanasiasa nchini kuanza kufanyia kazi matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 katika kuanga maendeleo..

Kutokana na hali hiyo, amesema kuwa ipo haja ya matokeo hayo kuanza kutumika kama dira ya kupanga mipango ya maendeleo kwa Taifa kuanzia katika ngazi ya chini kutokana na idadi ya watu walipo katika maneo yao.

Makinda ambaye pia Spika wa Bunge Mstaafu, ameyasema hay oleo Machi 13, 2024 Jijini Dar es Salaam, wakati akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari wa Mkoa wa Dar es Salaam  kuhusu matumizi ya takwimu za Sensa katika masuala ya habari.

“Tumewaambia wanasiasa wenzagu, sensa hii imefanikiwa. Lakini, kwenu ni kiboko, shangilieni lakini watu watakuwa wanauliza maswali kutokana na takwimu na maelezo yaliyomo kwenye matokeo ya sensa. Sisi tunafundisha mpaka chini kwa wananchi,” amesema Makinda.

Amesema kuwa kutokana na wananchi kupata uelewa kuhusu matumizi ya takwimu ikitokea kiongozi wa siasa anataka kusema vitu vyake visivyo na uhalisia, mtu wa kawaida atanyoosha mkono kumuumbua kufuatana na sensa.

Amebainisha kuwa NBS imeona umuhimuwa kuwapa mafunzo pia waandishi wa habari ili taaluma hiyo iwe ya kuaminika zaidi kwa takwimu.

Makinda amesema kuwa baada ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kutangaza matokeo hayo ya mwanzo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, ulitolewa mwongozo ktika kuwapo kwa uwazi na kupanua wigo ya matokeo hayo ya Sensa.

Katika mafunzo, imebainika kuwa Tanzania ina idadi kubwa ya wategemezi ambapo kati ya watu 100 watu 87 wana uwezo wa kufanya kazi lakini hawajishughulishi huku mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiongoza.

Hiyo ni kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi iliyofanyika mwaka 2022 ambapo imebaini Simiyu inaongoza kwa kuwa na wategemezi 119 ukifuatiwa na Tabora na Katavi 110 kila moja.

Mkoa wa Dar es Salaam umetajwa kuwa na uwiano mdogo wa wategemezi ambao ni 51.

Akizungumza Mtakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Omari Mdoka amesema takwimu zinaonyesha kuwa wenye umri wa miaka 15 hadi 64 ni tegemezi. Akitoa mchanganuo wa takwimu hizo, Mdoka amesema katika sensa ya mwaka 2022 mbali na Simiyu, Tabora na Katavi pia mikoa mingine ni Kigoma wategemezi 109, Rukwa 109, Mara 107, Geita 107 na Singida 105

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here