Home KITAIFA MBOWE AKWAA KISIKI MAHAKAMANI ‘ABWAGWA’ NA WAANDISHI KESI YA MADAI YA MISHAHARA

MBOWE AKWAA KISIKI MAHAKAMANI ‘ABWAGWA’ NA WAANDISHI KESI YA MADAI YA MISHAHARA

Google search engine

*NI KESI YA MADAI YA WAANDISHI WA HABARI

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe

Na MWANDISHI WETU

-DAR ES SALAAM

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Divisheni ya Kazi imetupilia mbali maombi ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kutaka waandishi wa habari 10 wanaomdai mtoto wake, Dudley Mbowe wamlipe gharama kwa kukamata nyumba yake.

Uamuzi huo wa Mahakama umetolewa leo Machi 13,2024 mbele ya Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Mary Mrio baada ya kupitia hoja za pande zote mbili.

Akisoma uamuzi huo, Msajili Mrio amesema mahakama baada ya kupitia maombi yaliyowasilishwa na Mbowe kupitia Wakili wake John Mallya, iliona kwamba hakuna ubishi katika maombi ya kuiachia nyumba.

Amesema kinachobishaniwa mahakamani ni mwombaji Mbowe kulipwa gharama za kesi na wajibu maombi.

“Mahakama iliangalia katika kesi hii gharama zilipwe au zisilipwe, nimepitia gazeti la Serikali (GN) namba 106 la mwaka 2007 ilielekeza kwamba kesi za aina hii hakuna sehemu inayoelekeza kulipa gharama.

“Mahakama inaona hakuna haja ya kutoa gharama, kila upande ubebe gharama zake, nyumba iliyokamatwa iko huru,”amesema Msajili Urio.

Waandishi hao 10 wanamdai Mkurugenzi wa TanzaiaDaima News Paper jumla ya Shilingi milioni  62.7 baada ya kushinda tuzo kutoka

Awali waandishi hao walishinda Tuzo iliyotolewa na CMA Ilala.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here