Home KITAIFA WANAFUNZI SAME WASAIDIWA TAULO ZA KIKE KUPUNGUZA UTORO SHULENI

WANAFUNZI SAME WASAIDIWA TAULO ZA KIKE KUPUNGUZA UTORO SHULENI

Google search engine
Mkuu wa Wilaya ya Same, Kasilda Mgeni (kushoto), akikabidhi taulo za kike kwa wanafunzo wa shule za Sekondari za Mighareni na Kwakoko wilayani Same mkoani Kilimanjaro. Msaada huo ni sehemu ya Maadhimisho wa Siku ya Wanawake Duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Machi 8 ya kila mwaka

Na ASHRACK MIRAJI

-SAME, KILIMANJARO

WANAFUNZI wa kike wa Shule za Sekondari Mighareni na Kwakoko wilayani Same mkoani Kilimanjaro, wamepatiwa taulo za kike bure zenye thamani ya Shiligi 700,000 ziwawezeshe kupunguza adha ya kushindwa kuhudhuria darasani wakati wa hedhi.

Hatua hiyo imebainika huku baadhi ya wanafunzi wanaotoka katika shule hizo ambao kila mara hushindwa kuhudhuria baadhi ya vipindi darasani wawapo katika kipindi cha hedhi kwa kukosa taulo za kike na kusababisha kuyumba kitaaluma.

Akikabidhi taulo za kike kwa baadhi ya wanafunzi wa shule za Mighareni na kwakoko, Mkuu wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni amewataka wananfuzi hao kujiepusha na masuala yanayopelekea mmomonyoko wa maadili pindi wanapokuwa nyumbani na kujikuta baadhi yao wakishindwa kufikia ndoto yao kwenye elimu.

 “Sisi wanawake tuna uwezo mkubwa sana lakini jitahidi sana kujiepusha na mambo yatakayowafanya msifikie ndoto zenu kwahiyo niwaombe sana mnapokuwa shuleni someni

“…fanyeni kile kilicho waleta shuleni wazazi wenu wanawategemea sana, chondechonde wanangu someni hayo mambo mengine mtakutana nayo baadae,” amesema DC Mgeni

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya amewaaka wanafunzi hao kuitumia vyema fursa iliyotolewa na Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ya elimu bure kuanzia ngazi ya msingi hadi sekondari.

Nao baadhi ya baadhi ya wanafunzi hao wanaosoma katika shule hizo, wamesema baadhi yao wanashindwa kuhudhuria vipindi darasani kwa kukosa taulo za kike ambapo huwalazimu kubaki nyumbani kwa siku tano mfululizo hadi wanapokuwa wamealiza hedhi.

Mmoja wa wanaunzi hao, Jenipher Mgonja amesema changamoto ya kukosa taulo za kike inasababisha wanafunzi hasa wa kike kuonekana kuwa watoro darasani na kushindwa kwenda shule na kuwalazimu kubaki nyumbani  kwa kukosa msaada wa kujisitiri.

“Tunamshukuru Mkuu wa wilaya ya Same, watumishi wanawake kutoka Ofisi ya Mkurugenzi na Mkuu wa Wilaya ya Same pamoja na wadau kutoka mashirika yasiyo ya kiserikali kwa kutupatia taulo za kikevkwani kabla ya hapo tulipata changamoto mbalimbal. Na wengine walishindwa kuhudhuria vipindi darasani kwa kukosa taulo za kike” amesema.

Ugawaji huo wa taule za kike ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo huadhimishwa kila Machi 8 duniani kote, ambapo Ofisi ya Mkurugenzi na Mkuu wa Wilaya ya Same kwa kushirikiana na wadau waliguswa na hilo na kuamua kuchangia taulo hizo za kike kama mkakati wa kusaidia kukuza elimu hasa kwa mtoto wa kike.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here