Home KITAIFA WAZIRI AWESO ASISITIZA MKAKATI WA KUWAJENGEA UWEZO WATENDAJI SEKTA YA MAJI

WAZIRI AWESO ASISITIZA MKAKATI WA KUWAJENGEA UWEZO WATENDAJI SEKTA YA MAJI

Google search engine
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, akizungumza wakati wa mahafali ya wahitimu wa Sekta ya Maji katika Chuo Kikuu cha AgroparisTech kilichopo Paris nchini Ufaransa

Na MWANDISHI WETU

-PARIS, UFARANSA

WAZIRI wa Maji,  Jumaa Aweso amefika katika Chuo Kikuu cha AgroparisTech kilichopo Paris nchini Ufaransa kwa mualiko maalum ikiwa ni pamoja na kushiriki mahafali ya kuhitimu kwa wataalamu wa Sekta ya Maji kutoka mataifa mbalimbali ambapo sehemu yao ni kutoka Tanzania wawili wakiwa Wakurugenzi watendaji wa Mamlaka za Maji za Lindi na Shinyanga, Mhandisi wa Maji kutola Mamlaka ya Maji Mwanza na Mhandisi wa Maji kutoka Wizarani.

Akizungumza mbele ya wahitimu hao,  Aweso amesema kipaumbele cha Wizara ya Maji ni kuendelea kuwajengea uwezo wataalam na watendaji wake ili wawe imara na mahiri kuendana na mabadiliko ya teknolojia.

Watumishi wa Sekta ya Maji katika chuo cha AgroparisTech kupitia ufadhili wa AFD kwa mpango maalum alioanzisha Waziri wa Maji wa kuwajengea watendaji uwezo.

Waziri Aweso ametumia wasaa huo kuomba ufadhili zaidi kwa watumishi wa Sekta ya Maji.

Pamoja  na hilo, Waziri Aweso ametembelea maeneo mbalimbali ya Chuo hiki na kujionea namna gani matumizi ya Teknolojia yanatumika katika kuimarisha sekta ya Maji.

Katika hatua nyingine Aweso amefanya mazungumzo na uongozi wa Chuo cha AgroParisTech na kutoa wazo la kuanzisha mashirikiano ya kimkakati kati yake na Chuo cha Maji cha Tanzania kilichopo chini ya usimamizi wa Wizara ya Maji.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here