Home KITAIFA TFS YAJIVUNIA MAENEO 12 MIAKA MITATU YA UONGOZI WA RAIS SAMIA MADARAKANI

TFS YAJIVUNIA MAENEO 12 MIAKA MITATU YA UONGOZI WA RAIS SAMIA MADARAKANI

Google search engine

*UKUSAYAJI MADUHULI WAZIDI KUIMARIKA, ASALI YA TABORA YABAMBA KWENYE MASOKO YA KIMATAIFA KWA UBORA

Kamishina Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Prof. Dos Santos, akielezea mafanikio ya TFS katika kipindi cha cha miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Sita, kwenye mkutano wa kikao kazi baina ya TFS na Wahariri wa vyomba vya Habari, kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR) na kufanyika Jijini Dar es Salaam.
Afisa Mwandamizi wa Habari na Mawasiliano kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR), Sabato Kosuri, akifafanua jambo wakati wa Kikao kazi baina ya TFS na Wahariri.

Na MWANDISHI WETU

-BEST MEDIA, DAR ES SALAAM

WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), umeeleza mafanikio 12 ya uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ambaye amesaidia kuleta mageuzi kwenye sekta ya hifadhi ya misitu nchini.

Kutokana na hali hiyo inatajwa kuwa miaka mitatu ya Rais Samia imesaidia kuongeza Rasilimali Misitu 464 ya ukubwa na ikolojia tofauti pamoja na kuongeza na idadi ya watalii nchini.

Akizungumza leo Machi 19, 2024 Jijini Dar es Salaam katika Mkutano wa wahariri wa vyobo vya habari ulioratibiwa na Msajili wa Hazina, Kamishna Mkuu wa Uhifadhi (TFS), Profesa Dos Silayo Santos, amesema kuwa Rais Dk. Samia, amefanya kazi kubwa ya kuongoza nchi ikiwemo kuboresha Sekta ya Maliasili na Utalii.

Amesema pamoja naye pia pongezi hizo wanastahili viongozi wa Wizara kwa usimamizi mzuri wa Sekta ya Maliasili zikiwemo Sekta ndogo za Misitu na Ufugaji Nyuki.

“Majukumu ya TFS kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Misitu na Sheria ya Ufugaji Nyuki, kukusanya maduhuli yatokanayo na mazao ya misitu, kutoa huduma za ugani katika maeneo ya Wakala, kuanzisha na kusimamia mashamba ya miti na manzuki,” amesema

Pamoja na hilo Kamishana wa Uhifadhi, Prof Santos, amesema kuwa TFS inasimamia misitu 464 ya Hifadhi inayojumuisha mashamba ya miti 24, misitu ya mazingira asilia (NFRs) 23, misitu yote ya mikoko kwenye mwambao wa Pwani ya Bahari(158,000 ha).

Pia wakala huo unasimamia vituo vya Malikale  sita Hifadhi za Nyuki 12 zenye uwezo wa kuzalisha (potential) 138,000t asali na nta 9,200t kwa mwaka.

“Hali ya sasa 30,000t za asali na tani 1,843 za nta kwa mwaka, wafugaji takribani milioni 1.2 pamoja na makundi (colonies) takriban 10m. pia vipo vito vya mbegu za mito vine,” amesema Prof. Santos

Amesema mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitatu ya Utawala wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha miaka mitatu Wakala umetekeleza shughuli mbalimbali na kupata mafanikio katika maeneo 12.

“Usimamizi wa rasilimali watu, usimamizi wa rasilimali za misitu, usimamizi na uendelezaji wa mashamba ya miti ya Serikali, kuendeleza utalii ikolojia na utamaduni, ufugaji nyuki, ukusanyaji wa maduhuli na mchango kwenye mfuko mkuu, maendeleo ya viwanda na biashara.

“…utekelezaji wa miradi ya maendeleo, kuimarisha mazingira ya kazi, kushirikishaji wa wadau katika uhifadhi, utalii na elimu kwa umma, huduma kwa jamii na utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya Taifa,” amesema

UBORA WA ASALI YA TABORA KIMATAIFA

Kamishna Santos, amesema kuwa uzalishaji wa mazao ya nyuki nchini umeongezeka hai kufikia wastani wa tani 32,691 toka 31,179 swa na ongezeko la asilimia tano huku asali ya Tabora ikiongoza kwa ubora kwenye masoko duniani.

Meneja Mawasiliano wa TFS, Johari Kachwamba, akifafanua jambo katika mkutano wa wahariri ulioratibiwa na Msajili wa Hazina leo Jijini Dar es Salaam

USIMAMIZI WA RASILIMALI WATU

TFS inasimamia rasilimali watu wanaojumuisha maofisa 643 na askari 1,454 jumla yao ikiwa ni 2097 katika kipindi cha Mwaka 2020/21.

“2023/2024 TFS iliajiri watumishi wapya 495. Watumishi 180 walipatiwa mafunzo ya muda mrefu na watumishi 1,481 ya muda mfupi katika fani mbalimbali,” amesema

UBORESHAJI MAZINGIRA YA KAZI, VITENDEA KAZI

Kamishna Santos amesema kuwa ununuzi wa magari na Mitambo Katika kipindi cha miaka mitatu Wakala umeweza kununua vyombo mbalimbali vya usafiri na mitambo yakiwemo magari 113, pikipiki 164, mitambo 17 kwa gharama ya Shilingi Bilioni 18.

UJENZI WA MAJENGO MBALIMBALI

Wakala umejenga majengo 88, zikiwemo ofisi 33, nyumba za watumishi 29, vituo vya ulinzi 26 na maghala ya kuhifadhia silaha nane  na ujenzi wa mifumo na Matumizi ya TEHAMA.

Baadhi ya wahariri wakimsikiliza Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Profesa Silayo Dos Santos (hayupo pichani)

USIMAMIZI WA MISITU

Kutokana na hali hiyo Prof Santos, amesema kuwa kupitia utekelezaji wa maelekezo ya BLM, migogoro 423 kati ya 438 baina ya hifadhi na vijiji na vitongoji imetatuliwa.

Kuhusu eneo la hifadhi yenye hekta 296,881 kwa ajili ya makazi, kilimo na ufugaji kwa wananchi lilitolewa sambama na kuendelea kutoa elimu ya uhifadhi na usimamizi wa misitu inaendelea kutolewa kwa jamii

“Kuimarisha mipaka kwa kuisafisha, kuweka vigingi na mabango ili kuzuia uvamizi katika maeneo ya hifadhi,”amesema

KUPANDISHA HADHI MISITU YA HIFADHI

Uhakiki mipaka ya misitu 55 yenye ukubwa wa hekta 1,453,025.846 ambayo ilianzishwa na kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali (GN).

Amesema misitu nane yenye ukubwa wa hekta 483,508.4 ilipandishwa hadhi kuwa hifadhi za misitu ya Mazingira Asilia.

Aliitaja misitu hiyo kuwa ni Itulu hills Pindiro , Pugu –Kazimzumbwi , Uzigua , Essimingori , Uvinza, East Matogoro na Hasama Hillls.

Prof. Santos amesema kuwa tathmini ya rasilimali za misitu (forest inventory) ilifanyika katika misitu 133 yenye ukubwa wa hekta 2,539,095.04 na kuandaliwa Mipango ya usimamizi (management plans).

“Juhudi hizo zinaendelea ambapo katika mwaka wa fedha 2023/2024 itaandaliwa mipango ya misitu 56 yakiwemo mashamba ya miti 14,” amesema

Ameema pia anakabiliana na majanga ya Moto Pori juhudi za kujikinga na moto pori katika hifadhi za misitu zimefanyika kwa kusafisha mipaka na njia za moto zenye urefu wa kilomita 13,426 pamoja na kutoa mafunzo ya mbinu za kukabiliana na kuepusha matukio ya moto kwa wananchi zaidi ya 29,685 katika vijiji 749 vinavyozunguka misitu 120.

Licha hilo amesema pia huanzisha na kutoa mafunzo kwa vikosi vya kukabiliana na matukio ya moto vyenye jumla ya watu 365

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es Salaam (DCPC), Samson Kamalamo akiuliza swali kwa Kamishna Santos (hayupo pichani)

IDADI YA WATALII NA MAPATO

Kamishna Prof Silaya, amesema kuwa juhudi zilizofanyika zimewezesha kuongezeka kwa idadi ya watalii wanaotembelea vituo vya utalii ikolojia kutoka 59,606 mwaka 2020/2021 hadi 242,824 mwaka 2022/2023 na mapato katika kipindi hicho yaliongezeka kutoka Shilingi 154,965,050 hadi kufikia wastani wa Shilingi Bilioni 1.5.

Amesema hayo ni mafanikio makubwa kupatikana na Wakala katika sekta ya utalii eneo la utalii ikolojia kuliko wakati mwingine wowote.

Amesema Wakala umejiwekea malengo ya kuweka rekodi mpya kwa kufikisha watalii 500,000 na kukusanya Shilingi bilioni tatu ifikapo mwaka 2025

UTANGAZAJI UTALII

Prof Santos amesema kuwaWakala umeendelea kutangaza vivutio vya utalii kupitia maonesho mbalimbali ya ndani na nje ya nchi ikiwemo Sabasaba, Nanenane, Tanga Trade Fair, International Tourism Expo Japan 2022, East Africa International Tourism Expo, S!TE na 2022 World Cup.

Amesema ubunifu wa mazao mapya ya utalii kama vile mashindano ya maarufu ya West Kili Forest Tour Challenge, Bata Msituni Festival, Magamba Walkathon, Swahili Marathon, Meru Forest trail Run, Rubare Marathon, Mkeka na Khanga Festival na Sao Hill Forest Rally

UKUSANYAJI MAPATO

Katika kipindi cha miaka mitatu, Wakala umekusanya jumla ya Shilingi Bilioni 371.9  na kfanikiwa kutoa gawio kwa Serikali kiasi cha Shilingi Bilioni 62.9 ikiwa ni asilimia 15 ya makusanyo.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here