Home BIASHARA WAZIRI DK. ASHATU KIJAJI KUFUNGUA SEMINA YA DCTS MACHI 28, 2024 JIJINI...

WAZIRI DK. ASHATU KIJAJI KUFUNGUA SEMINA YA DCTS MACHI 28, 2024 JIJINI DAR ES SALAAM

Google search engine
Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji

NA ANDREW CHALE

-DAR ES SALAAM

WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Semina maalum kuhusu Mpango wa Biashara wa nchi ya Uingereza na Nchi zinazoendelea (UK Developing Countries Trading Scheme – DCTS) itakayofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa jijini Dar es Salaam, Machi 28, 2024, kuanzia saa 3:00 asubuhi.

Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa kwa Vyombo vya habari na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Semina hiyo ina lengo la kufahamisha wadau wa biashara  nchini juu ya fursa ya mauzo ya bidhaa za Tanzania katika soko la Uingereza kupitia Mpango wa Serikali ya Uingereza wa Kufanya Biashara na nchi zinazoendelea na inatarajiwa kufungwa na Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda wa Serikali za Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Omar Said Shabaan.

“Mpango wa DCTS  ulizinduliwa Mei, 2023, ambapo Tanzania ni miongoni mwa nchi 65 ambazo Uingereza imezijumuisha katika mpango huo ili kuweza kuuza bidhaa zake bila kulipa ushuru na imeingia pia katika kundi la nchi ambazo asilimia 99 ya bidhaa zake zitanufaika na msamaha wa kodi.

“Lakimi pia, Semina hiyo ina lengo la kufahamisha wadau wa biashara  nchini juu ya fursa ya mauzo ya bidhaa za Tanzania katika soko la Uingereza,” imeeleza taarifa hiyo.

Walengwa wa semina hiyo ni wadau wa biashara wenye nia ya kuuza bidhaa za aina mbalimbali katika soko la Uingereza ambapo Wadau wanaweza pia kushiriki katika Semina hiyo kwa njia ya mtandao, kupitia link maalum ya mtandao wa “Teams” itakayotolewa kwa watakaojisajili kupitia:https://docs.google.com/forms/d/e/1FAIpQLSdjoGDLwkXfu9PWlV7Oc3LOnn5tRyELsimZVUaMaFhCGFB1Mw/viewform.

 Aidha, imebainisha kuwa, Wananchi wote wanaweza kuifuatilia Semina hiyo kupitia na chaneli ya YouTube ya Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza ijulikanayo kama Ubalozi London (http://www.youtube.com/@ubaloziLondon).

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here