Na MWANDISHI WETU
-ARUSHA
MKURUGENZI wa Mashtaka nchini DPP amemfutia kesi na kumfungulia mpya mbili za uhujumu uchumi aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Dk. John Pima na wenzake watatu.
Kesi hizo zimefunguliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, zikimkabili na wenzake watatu.
Kesi hizo zina mashtaka nane kila moja ikiwemo ya ufujaji na ubadhirifu wa milioni 65 fedha za Serikali.
Katika maelezo ya kesi inadaiwa walijipatia kiasi hicho kwa kutumia nyaraka kumdanganya mwajiri kuwa wamezitumia fedha hizo kumwaga Moramu katika Masoko ya Kilombero, Soko Kuu, Mbauda na Morombo jambo ambalo sio kweli.
Washtakiwa wote wamekana mashtaka huku watatu wakiachiwa kwa dhamana.