MWANDISHI WETU
-DODOMA
JUMLA ya Sh milioni tano na zawadi nyingine za furaha,kofia na mavazi kwa ajili ya Mama Lishe jana zilikwenda kwa wateja wa NMB Benki waliofungua akaunti ya NMB pesa, ‘Haachwi mtu’.
Kiasi hicho ni sehemu ya zawadi nyingi ambazo hutolewa na NMB katika mpango wao wa ‘Weka na Ushinde’ ambao ulianzakuchezeshwa Mwezi Februari 2024 na unatarajia kukamilika Mei mwaka huu ambapo washindi watajinyakulia fedha taslimu Shilingi milioni 10, Shilingi milioni tatu ,Pikipiki ya miguu mitatu, friji, mitungi ya gesi na luninga.
Meneja wa NMB Tawi la Mazengo Jijini Dodoma, Victor Dilunga amesema kuwa, zawadi zilizotolewa ni sehemu ya fedha Shilingi milioni 150 ambazo benki hiyo imetenga kwa ajili ya wateja wake kwenye shindano hilo ambalo jana liliingia hatua ya sita.
Dilunga amesema kwenye droo hiyo wamekuwa wakichezesha na kuwapata washindi kwa kila wiki,mwezi na kubwa kuliko yote itakuwa ni ile ya mwisho ambayo ndiyo imebebakitita kikubwa kuliko vyote tangu walipoanza mpango huo.
“Leo tumepata washindi 10 ambapo kila mmoja amejinyakulia Shilingi 500,000 na tumechezesha kwa uwazi kila mmoja ameshuhudia,urahisi wa kufungua akaunti hii ni mtu kuwa na Shilingi 1000 na kitambulisho cha NIDA au namba yake tu,” amesema Dilunga.
Meneja huyo amesema baada ya kufungua akaunti hiyo, mteja anapaswa kuweka Shilingi 50,000 na moja kwa moja atakuwa ameingia kwenye droo hiyo ambayo inamwezeshakugombania sehemu ya Shilingi milioni 150 zilizotengwa kwenye shindanozima.
Kwa upande wake Afisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Ibrahimu Sikana, amesema washindi wanaopatikana kupitia mashindano mbalimbali ndani ya NMB wapo kihalali kwani benki hiyo inafuatamasharti na sheria za michezo ya kubahatisha kila inapochezesha droo zake.
Sikana ameipongeza benki hiyo kwa kufuata taratibu na kanuni za uchezeshaji wa michezo ya kubahatisha na kutaka taasisi zingine zifuate au kuiga namna wanavyofanya kwani inasaidiakuondoamlalamiko na manung’uniko kwa wanaokosa.
Pamoja na hali hiyo pia amesisitiza kwa NMB kuendelea na mfumo uliopo kwa sasa ili waendelee kuaminika akisema ndiyo njia pekee inayowapa heshima ya kuaminiwa na taasisi kubwa kwenye matunzo ya fedha za Watanzania.
Naye Meneja Mauzo wa NMB Makao Makuu, Janeth Nyamko amesisitiza wananchi kuendelea kuiamini benki hiyo ambayo imejipambanua kwa kufanya mambo makubwa yenye tija kwa wananchi na mara nyingine imekuwa sehemu ya kuwapa faraja Watanzania.
Janeth amesema awamuijayo droo itachezeshwa kwenye Tawi la Wami lililoko mjini Morogoro kwani ni utaratibu waliojiwekea ni kwamba michezo hiyo inachezeshwa kwa mzunguko kwenye matawi kwa nchi nzima.