Home KIMATAIFA RAIS TINUBU WA NIGERIA APIGA ‘STOP’ SAFARI ZA NJE YA NCHI

RAIS TINUBU WA NIGERIA APIGA ‘STOP’ SAFARI ZA NJE YA NCHI

Google search engine
Rais wa Nigeria, Bola Ahmed Tinubu

Na MWANDISHI WETU

-ABUJA, NIGERIA

RAIS wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu atangaza marufuku ya miezi mitatu kwa mawaziri na maafisa wengine wa serikali kwenda safari za nje zinazofadhiliwa na umma kuanzia Aprili mosi, 2024.

Uauzi huo waTinubu umekuja siku chache baada ya wapinzani wake akiwamo asimu wake mkuu wa kisiasa Abubakar Atiku kumwita ‘Vasco Dagama’ kutokana na kuwa na utitiri wa safari nje ya nchi kwa ktumia feda za walipakodi huku shughuli muhimu za kijamii zikihitaji kutatua changamoto zao na vongozi ambao kila mara husafiri nje ya Nigeria na kubeba idadi kubwa ya maofisa kwenye misafara yao.

Rais Tinubu, katika barua yake aliyoiandika, aliagiza kuzuiliwa kwa safari zote za nje, lakini akasema kwamba ruhusa inaweza kutolewa kwa safari zinazoonekana kuwa muhimu sana.

Barua hiyo iliongeza kuwa Tinubu alisema ruhusa hiyo itahitaji idhini ya rais ambayo lazima itafutwe wiki mbili kabla ya safari iliyopangwa.

Kutokana na barua hiyo, marufuku hiyo itadumu kwa siku 90 kwa mara ya kwanza na itaanza kutumika Aprili 1, 2024.

Mkuu wa wafanyikazi wa Tinubu amesema hatua hiyo ilichochewa na “wasiwasi wa rais kuhusu kupanda kwa gharama za usafiri”. Marufuku hiyo itaanza kutekelezwa Aprili 1, 2024.

Rais Tinubu na utawala wake wamekuwa wakikosolewa na baadhi ya watu kwa ziara zao za mara kwa mara nje ya nchi.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here