Home KITAIFA SHIRIKA LA KDI LAANDAA FUTARI KWA VIONGOZI WA JUMUIYA YA MARIDHIANO NA...

SHIRIKA LA KDI LAANDAA FUTARI KWA VIONGOZI WA JUMUIYA YA MARIDHIANO NA AMANI (JMAT)

Google search engine
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT) Sheikh Alhad Mussa Salum

Na MWANDISHI WETU

-KILIMANJARO

SHIRIKA lisilo la Kiserikali la Kilimanjaro Dialogue Institute (KDI) la Jijini Dar es Salaam linalofanya shughuli za kukuza na kudumisha amani na maridhiano limefanikiwa kuandaa futari kwa ajili ya viongozi wa Kiislamu ambao wanafunga Mwezi Mtukufu wa Ramadhan pamoja na Mfungo wa Kwaresma kwa Wakristo.

Tukio hilo limefanyika Maachi 24, 2024 ambapo mgeni rasmi alikuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT) Sheikh Alhad Mussa Salum, ambapo ujumbe katika futari hiyo ilikuwa “Karamu ya Amani:

Akizungumza katika tukio hilo, Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Ibrahim Yunus amesema suala la amani na utulivu wa ni wajibu wa jamii kuhakikisha inakuwapo wakati wote.

Kutokana na hali hiyo alimewataka viongozi na wananchi waliohudhuria Iftari hiyo kushirikiana na Serikali kama mkakati wa kuilinda amani na utuluvu ulipo nchini.

 “Tunafurahi kwa Taasisi ya KDI kuandaa tukio hili lenye maana ambalo linaadhimisha utajiri wa mila zetu tofauti za kidinina linaendana na dira ya upendo na maridhiano aliyotutengenezea Rais wetu, Mama yetu Mheshimiwa Dk. Samia Suluhu Hassan,” amesema Yunus

Kwa upande wake Mwenyekiti wa JMAT, Sheikh Alhad Mussa Salum, ambaye alikuwa ameambatana na Mwenekiti wa jumuiya hiyo Mkoa wa Dar es Salaam, Mchungaji Christosiler Kalata, tukio hilo linakwenda kuleta umoja na mshikamano kwa waumini wa dni zote mbili nchini.

 “Kwa kukutana pamoja kwa chakula cha pamoja, tunatumai kuendeleza uelewa na thamani ya imani za kila mmoja, kukuza jamii yenye kujumuisha, yenye umoja, amani na maridhiano zaidi,” amesema

Tukio hilo lilifanyika kwa msaada wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya ISHIK na Taasisi ya Umoja wa Wafanyabiashara ya Tanzania Global Business Initiative.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here