Home KIMATAIFA WANAWAKE WANNE WAUAWA NIGERIA KATIKA MIKANYAGANO YA KUPEWA PESA

WANAWAKE WANNE WAUAWA NIGERIA KATIKA MIKANYAGANO YA KUPEWA PESA

Google search engine

-BAUCHI, NIGERIA

MIKANYAGANO ya kupewa pesa na chakula bila malipo imekuwa jambo la kawaida Nigeria huku ikikabiliwa na mzozo mkubwa wa kupanda kwa gharama za maisha.

Takriban wanawake wanne wameuawa nchini Nigeria katika mkanyagano huku umati wa watu uking’ang’ania kupata pesa kutoka kwa mfanyabiashara, polisi wamesema.

Msichana mwenye umri wa miaka 17 pia alijeruhiwa katika tukio la Jumapili lililotokea Kaskazini Mashariki mwa Jimbo la Bauchi.

Ripoti zingine zinaweka idadi ya waliofariki kuwa juu zaidi.

Mfanyabiashara huyo alikuwa akitoa Naira 5,000 (Dola 3) kwa kila mpokeaji ili kuwasaidia kununua chakula wakati wa mwezi mtukufu wa Kiislamu unaoendelea wa Ramadhani, shirika la habari la AFP liliripoti.

Raia wa Nigeria wamekuwa wakikabiliana na changamoto kali za kiuchumi, ikiwa ni pamoja na kupanda kwa bei ya vyakula.

Wanafunzi wawili wa Chuo Kikuu cha Jimbo la Nasarawa karibu na mji mkuu Abuja walifariki siku ya Ijumaa wakati wa mkanyagano walipokuwa wakipewa mchele bila malipo.

Takriban vifo saba viliripotiwa katika kitovu cha kibiashara cha Lagos mwezi uliopita baada ya mvutano wa kupata mchele wa bei nafuu uliokuwa ukiuzwa na Huduma ya Forodha ya Nigeria. Polisi wameonya dhidi ya kushikilia michango ya umma bila utaratibu mzuri wa kudhibiti umati kutoka kwa mamlaka

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here