Home KITAIFA RIPOTI YA CAG YABAINI MAZITO DENI LA TAIFA

RIPOTI YA CAG YABAINI MAZITO DENI LA TAIFA

Google search engine

*AIBUA MENGINE ATCL, TTCL, MSD, TANESCO YAGUSWA SAKATA LA MITA TAKUKURU NAO WANUSA VIASHIRIA VYA RUSHWA MAJALADA 156

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akipokea Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2022/23 kutoka kwa Charles Kichere Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 28 Machi, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akipokea Taarifa ya Utendaji Kazi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa mwaka 2022/2023 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo CP. Salum Hamduni Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma Machi 28, 2024.

Na MWANDISHI WETU

-DODOMA

RIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2022/23 imeoyesha kuwepo kwa ongezeko la deni la Taifa kwa asilimia 15 kutoka Shilingi trilioni 71.31 mwaka 2021/22 hadi Sh trilioni 82.25 Juni 30, 2023. Deni hilo linajumuisha deni la ndani Sh trilioni 28.92 na deni la nje Sh trilioni 53.32.

Hayo yamesemwa leo Machi 28, 2024 Ikulu ya Chamwino Jijini Dodoma wakati akitoa tathmini ya hasara zilizotokea kwenye taasisi mbalimbali za umma na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere, wakati akitoa ripoti ya ukaguzi kwa mwaka 2022/23 mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Kutokana na hali taarifa hiyo ya ukaguzi imesema kipimo cha deni la Serikali kinaonyesha kuwa deni hilo ni himilivu na kwamba uwiano wa kulipa mdeni na mauzo ya nje ni asilimia 12.7 chini kidogo ya kiwango cha ukomo cha asilimia 15 na uwiano wa malipo yya deni na mapato ni asilimia 14.3 chini kidogo kiwango cha ukomo elekezi cha asilimia 18.

HASARA ATCL

Kuhusu hali ndani ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), CAG Kichere, amesema kuwa kwa mwaka wa fedha 2022/23, limepata amebaini hasara hasara ya Shilingi bilioni 56.64, ikiwa imeongezeka kwa asilimia 61 kutoka Shilingi bilioni 35.4 ya mwaka uliotangulia.

WINGU TTCL

Katika ripiti hiyo ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere amesema kuwa amebaini Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limepata hasara ya Sh894 milioni licha ya kupokea ruzuku ya Shilingi bilioni 4.55 kutoka serikalini.

Hata hivyo amesema kuw hasara kwa shirika hilo imepungua kwa asilimia 94. CAG amesema shirika hilo limerejesha Shilingi bilioni 4.4 kutoka kwenye ruzuku hiyo kama mapato yake kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

MSD NA MANUNUZI WA UVIKO

Kichere amesema Bohari ya Dawa (MSD) ilifanya manunuzi ya vifaa vya Uviko-19 bila ushauri wa kiufundi na kusababisha vifaa hivyo kutofaa kwa matumizi, baada ya kukaguliwa na wataalamu.

Amesema ingawa MSD ilishalipa fedha hizo, anapendekeza hatua zichukuliwe kwa wafanyakazi ambao walihusika pamoja na kurejesha fedha hizo za umma.

MITA ZA UMEME

Akiwasilisha Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Charles Kichere amesema jumla ya mita za umeme 108,088 zimebadilishwa Tanesco kabla ya uhai wake kuisha huku baadhi zikiwa zimekaa muda mfupi kwenye matumizi.

Akiwasilisha taarifa ukaguzi wake kwa mwaka 2022/23 amesema kitendo hicho ni kinyume na kanuni ya muda wa matumizi ya mita, ambao ni miaka 20.

KAULI YA TAKUKURU

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Salum Hamduni amesema jumla ya majalada 156 kati ya 375 yaliyofunguliwa kutokana na ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikiali (CAG) mwaka 2021/22 yaliyoonekana kuwa na viashiria ya jinai na rushwa yalikosa ushahidi.

Hamduni amesema hayo wakati akiwasilisha ripoti ya utendaji kazi wa Takukuru kwa mwaka 2022/23 Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here