Na MWANDISHI WETU
-BEST MEDIA, DAR ES SALAAM
BAADA ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, kuwateua makatibu wa Jumuiya za Vijana, Wazazi na aliyekuwa Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Paul Makonda kushika nafasi Serikalini sasa ni wazi mabadiliko ya sura mpya kwenye Sekreterieti yananukia.
Kutokana na hali hiyo leo Machi 31, 2024, Rais Dk. Samia, amefanya uteuzi wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Vijana, Fakii Lulandala kuwa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara pamoja na mwenzake wa Wazazi Gilbert Kalima kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga sasa ni wazi nafasi hizo zinapata sura mpya.
Lulandala ambaye aliteuliwa Oktoba 1, 2023 kushika wadhifa huo akitolewa kwenye ukuu wa Wilaya ya Momba mkoani Songwe ambeye amehudumu kwenye nafasi hiyo wa miezi mitano hadi anateuliwa tena kushika nafasi ya ukuu wa wilaya.
Hatua hiyo inatajwa kuwa ni sehemu ya mabadiliko ya kawaida katika kujipanga kuelekea kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu pamoja na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Pamoja na hali hiyo pia inamlazimu katika siku za hivi karibuni Mwenyekiti wa CCM Rais Samia Suluhu Hassan kuteua tena Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo baada ya aliyeuliwa kushika nafasi hiyo, Paul Makonda Oktoba 22 ya mwaka huu 2023 ambaye naye ametumikia nafasi hiyo kwa miezi mitano.
Uamuzi wa CCM wa kumrejesha kada wake Paul Makonda katika medani za uongozi baada ilieleza ni kama hatua ya kujipanga japo taarifa kutoka ndani ya CCM wapo baadhi ya wahafidhina ambao walikuwa wakipinga chinichii hatua uteuzi huo na wengine kudai utakweda kutonesha majeraha ya kisiasa kwa kile kilichoelezwa rekodi ya uongozi wa mwanasiasa huyo wakati akihudumu kwenye nafasi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Kwa upande wa majina ambayo yamekuwa yakitajwa huenda yakaingia kwenye majadala ya uteuzi kwa nafasi ya Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wapo makada kadhaa wa CCM wanaotajwa huku jina la Amos Makalla nalo likichomoza kwenye nafasi hiyo.
“Makalla aliwahi kuwa mchumi wa CCM akichukua mikoba ya Rostam Aziz hivyo kwa kuwa ametolewa kwenye ukuu wa mkoa tangu mwanzo naye amekuwa akitajwa sana kwenye nafasi hii kwa kuwa anaimudu vizuri na chama anakijua vema.
“Ila kwa maana nafasi hiyo pia wapo wengi kama Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila naye anasifa kubwa ya kuwa Mwenezi mwenye uwezo mkuwa pia. Kwa kuwa ni suala la muda acha tusubiri kwanza nini maamuzi ya chama.
“…Sekreterieti sasa inakwenda kusukwa upya, huwezi kuwa na Katibu Mkuu mpya kama mwanadiploasia Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi halafu CCM inashindwa kirahisi hilo sahau kabisa. Katika nyakati zote za CCM hakika sasa mama Samia anafanya kazi kubwa,” amesema Mzee Simba Marijani ambaye ni kada wa CCM