Home KITAIFA MAKALLA ATUMA UJUMBE KWA ‘WANAOMBEZA’

MAKALLA ATUMA UJUMBE KWA ‘WANAOMBEZA’

Google search engine

*ASEMA KAZI ANAYOFANYA NDANI YA CCM SI NGENI KWAKE, ATAMBA KUTAMBUA MAJUKUMU YAKE

Katibu wa Halmashauri Kuu, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla, akizungumza kwenye mapokezi leo Jijini Da es Salaam

Na MWANDISHI WETU

-DAR ES SALAAM

Katibu wa Halmashauri Kuu, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla ametuma ujumbe kwa watu wanaombea kuteliwa kwake kwenye nafasi hiyo na kuweka wazi kwamba jukumu hilo si geni kwake ndani ya chama.

Kutokana na hilo amesema kuwa anajua wajibu wake na nini anachotakiwa kufanya kwa mujibu wa Katiba ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanaoandika kwenye mitandao ya kijamii ni sawa tu wanamkumbusha wajibu ambao pia naye anautambua.

Hayo ameyasema leo Aprili 5, 2024 Lumumba katika mapokezi yaliyoandaliwa na CCM Mkoa wa Dar es Salaam ambapo wajumbe hao wapya wa Sekreterieti mpya ya CCM walipokelewa na mamia ya wanachama wa chama hicho tawala.

Makalla na wnzake waliteuliwa Aprili 3, 2024 na Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. Samia Suluhu Hassan akichukua mikoba ya mtangulizi wake Paul Makonda ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

“Leo nimekabidhiwa mikoba kutoka kwa mdogo wangu (Paul Makonda aliyekuwa Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa, ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha), amenikabidhi ofisi, watumishi wa idara na makabrasha ambayo yamejaa majukumu yote, ikiwemo kazi alizozifanya.

“Tunamshukuru kwa mchango wake alioufanya katika chama chetu na tunamtakia kila la heri katika nafasi aliyoipata ya kuwa Mkuu wa Mkoa, sisi tutaendelea kumpa ushirikiano wa chama katika kazi zake, lakini pia ameingia kwenye record (kumbukumbu) za makatibu wa uenezi waliofanya kazi Chama Cha Mapinduzi (CCM), tunaheshimu sana mchango wake na mimi nitaanzia pale alipoishia kukieneza chama chetu.

“Ninaposema nimerudi nyumbani mjuwe kuwa naelewa majukumu ya Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa maana nasoma mitandaoni, kuna watu baadhi wananikumbusha majukumu sasa nawaambia kwamba nayaelewa, majukumu yangu yako katika Katiba ya chama cha Mapinduzi (CCM) Ibara ya 107 kifungu cha 2 (a, b, c, d, mpaka f) yanaeleza majukumu ya nafasi niliyonayo,” amesema Makalla

Amesema sasa ni jukumu leo kwenda ngazi ya chini kusikiliza na kutatua kero za wananchi wakiwamo wanachama wa chama hicho kuanzia ngazi ya mashina.

MONGELA

Naye mgei rasmi katika mapokezi hayo Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mongela, amesema kuwa yeye kwa nafasi yake si mtu wa kuzungumza sana ila ameahidi kuimarisha masuala ya utendaji kwa watumishi wa chama hichi kuanzia Taifa hadi kwenye mashina.

ALLY HAPI

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Ally Hapi, amewataka wana CCM kujipanga kuelekea kuitafuta dola kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu mwakani.

“Naomba wakati huu ambao tunaingia kwenye mapambano niwaambie wale jamaa wa upande wa pili (vyama vya upinzani), ambao kazi yao ni kelele tu, Rais (Samia Suluhu) amewatengenezea mazingira mazuri wanafanya mikutano, wanafanya shughuli zao nyingine, wamepewa ruzuku lakini shukrani hawana, na niliwasikia wengine wanalalamika kwenye uchaguzi mdogo wanasema kwamba mbona hawajatuachia, yaani CCM ifanye kazi ya kuwaachia kata kweli?

“…wasitegemee huruma uchaguzi ni kazi na malengo yetu ni kuendelea kushika dola, na sisi tuko tayari kuendelea kukiendesha chama chetu, muda wa kuoneana huruma umekwisha, mikutano wote tunafanya, kujipanga wote tunajipanga habari za kubebwa hazipo, twende kwa wananchi tukatafute kura, twende kwa wananchi tukarejeshe na kuongeza heshima ya ushindi wa CCM,” amesema Hapi

Juzi, Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) chini ya uenyekiti wa Rais Samia Suluhu Hassan ilikaa jijini Dar es Salaam na kufanya uteuzi wa viongozi kujaza nafasi zilizoachwa wazi na baadhi ya viongozi wa sekretarieti walioteuliwa serikalini.

Walioteuliwa na NEC na nafasi zao ni John Mongela, Naibu Katibu Mkuu – Bara, Amos Makalla (Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo), Ally Hapi (Katibu wa Jumuiya ya Wazazi) na Jokate Mwegelo (Katibu wa Umoja wa Vijana), wote wanaunda sekretarieti inayoongozwa na Katibu Mkuu, Dk. Emmanuel Nchimbi.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here