Home KITAIFA TANAPA YANG’ARA TUZO ZA UMAHIRI MAWASILIANO

TANAPA YANG’ARA TUZO ZA UMAHIRI MAWASILIANO

Google search engine

Na MWANDISHI WETU

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kupitia Idara ya Mawasiliano imeshinda tuzo ya Umahiri katika Mawasiliano ya umma iliyobeba dhima ya “The Best use of Influencers Category for the year 2023”, hafla iliyofanyika usiku wa Aprili 5,.2024 katika Ukumbi wa St. Peter’s jijini Dar es Salaam, tuzo ambazo zimetolewa na Taasisi ya Public Relations Society of Tanzania (PRST).

Mgeni rasmi katika utoaji wa tuzo hiyo alikuwa Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari – Mhandisi Maryprisca Winfred Mahundi.

Ushindi huo umetokana na mchango mkubwa unaotolewa na Idara ya Mawasiliano – TANAPA katika kuhabarisha umma masuala mbalimbali ya Uhifadhi na Utalii.

Idara ya Mawasiliano- TANAPA imekuwa daraja la kuiunganisha taasisi hiyo na umma, hivyo tuzo hiyo itakuwa ni chachu ya kuimarisha mahusiano kati ya TANAPA, Serikali, vyombo vya habari na wadau mbalimbali

TANAPA ka sasa limekuwa jicho la nchi kwa kuwa Taasisi inatoa mchango mkubwa kuingiza fedha za kigeni na kuchochea ukuaji wa uchumi kwa kasi kupitia sekta ya utalii nchini.

Watoa Shukrani zao za dhati kwa Serikali ya Awamu ya Sita chini Rais Dk.Samia kwa kuongeza hamasa katika sekta ya utalii na kuitangaza Kimataifa kupitia Filamu ya Royal Tour.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here