Home KITAIFA RC SONGWE DANIEL CHONGOLO AKUTANA NA UONGOZI WA HIFADHI YA NGORONGORO

RC SONGWE DANIEL CHONGOLO AKUTANA NA UONGOZI WA HIFADHI YA NGORONGORO

Google search engine

Na MWANDISHI WETU

Uongozi ya Hifadhi ya Ngorongoro umefanya ziara ya kikazi kuonana na Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel  Chongolo.

Pamoja na mambo mengine walijadiliana kwa kina kuhusu Uendelezaji wa Eneo la Kimondo Kwa ajili ya Maendeleo ya Kitalii na kiuchumi.

Ili kufikia azma hiyo Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo ameiagiza Menejimenti ya Ngorongoro kuhakikisha inatenga Bajeti na kuwalipa Fidia Wananchi walio chukuliwa eneo la Kimondo kabla ya uendelezaji wa eneo la kitalii.

Katika hilo Menejimenti ya Ngorongoro imemhakikishia Mkuu huyo wa Mkoa kuwa mwaka wa fedha 2024/2025 imepanga Bajeti kwa ajili ya kulipa fidia wananchi waliopo karibu na eneo la kimondo katika kijiji cha Ndolezi Kata ya Mlangali Halmashauri ya wilaya ya Mbozi mkoani Songwe.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here