Home KITAIFA MADAKTARI WA WANYAMA NCHINI WATOA CHANJO KWA WANYAMA MKOANI IRINGA

MADAKTARI WA WANYAMA NCHINI WATOA CHANJO KWA WANYAMA MKOANI IRINGA

Google search engine
Madaktari wa Wanyama wakiendesha zoezi la utoai chanjo kwa mbwa mkoani Iringa, ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Madaktari wa Wanyama Duniani

Na MWANDISHI WETU

-IRINGA

CHAMA cha Madaktari wa Wanyama (TVA), kimeadhimisha Siku ya Madaktari wa Wanyama Duniani kwa kutoa chanjo kwa wanyama mbalimbali ikiwa ni njia ya kuwakinga na magonjwa mbalimbali ikiwamo sotoka na kichaa cha mbwa.

Pamoja na hali hiyo madaktari hai waliendesha uchunguzi wa wanyama na kuwapatia matibabu kama njia ya kuongeza tija kwenye maadhimisho hayo yanayofanyika kila mwaka ambapo kwa mwaka huu yalifanyika mkoani Iringa.

Akizungumza kuhusu maadhimso hayo kwa mwaka huu, Katibu wa chama hicho Kanda ya Nyanda za Juu Kusini  ambaye pia ni Meneja wa Kituo cha TVLA Iringa, Dk. Geoffrey Mbata amesema ugonjwa wa sotoka unawapata mbuzi na kondoo na chanjo kwa mbwa na paka ni dhidi ya ugonjwa wa kichaa cha mbwa.

“Kwa mwaka huu maadhimisho haya hufanyika Aprili 27, ya kila mwaka na mwaka huu tulikuwa hapa mkoani Iringa na kaulimbiu yetu ni Madaktari wa Wanyama ni wahudumu muhimu wa afya . Hivyo tumekuwa na shughuli kadhaa katika kuadhimisha siku hii katika maeneo ya Wilaya za Iringa, Wilaya ya Kilolo na Halmashauri ya Iringa,” amesema Dk. Mbata

Daktari huyo wa Wanyama, amesema kuwa ni lazima jamii itambue kwamba kuna umuhimu wa kuchanja wanyama kwani inadhibiti ueneaji wa magonjwa ili kupata mazao bora, salama na yenye afya ikiwamo mayai, maziwa na nyama.

Dk. Mbata amesema kuwa kutokana umuhimu huo ni lazima kutoa matibabu na chanjo kwa wanyama nchini kama njia kuwakinga na magonjwa hayo ambapo kama yasipodhibitiwa yanaweza kuleta madhara kwa wanyama na binadamu.

“Tumefanya upasuaji mdogo kwa wanyama kama vile utoaji wa kizazi kwa mbwa na paka na huduma hizo zimefanyika bure kwa wafugaji wa maeneo husika,” amesema

Kutokana na hali hiyo amesema kuwa huduma hizo hutolewa na madaktari wa wanyama, madaktari wasaidizi na kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ikiwemo Shirika la Chakula Duniani (FAO).

Katika maadhiisho hayo Dk. Mbata amesema kuwa wamefanikiwa kutoa elimu hasa kwa wanafunzi juu ya umuhimu wa uwepo wa madaktari wa wanyama nchini na Duniani.

Ameeleza kuwa lengo la kuwepo kwa maadhimisho hayo ni kueleza umuhimu wa madaktari wa wanyama kwani jamii haitambui umuhimu wa madaktari hao.

Madaktari wa Wanyama akitoa elimu kwa wanafunzi wa shue za msingi Mjini Iringa, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho hayo

“Tukiwa hapa Iringa tumefanikiwa kutembelea shule tatu katika Manispaa ya Iringa kuhusu kueleza umuhimu wa madaktari wa wanyama katika udhibiti magonjwa,” amesema na kusisitiza Dk. Mbata

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here