Na MWANDISHI WETU
-DODOMA
BENKI ya NMB imewahakikishia Watanzania kuwa huduma zake zitaendelea zitaendelea kutolea saa 24 kwani lengo ni kuwaondolea usumbufu wateja.
Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa NMB tawi la Mazengo (Dodoma) Victor Dilunga wakati akiwasilisha mada kwenye Mkutano Mkuu wa 13 wa Mwaka wa Kitaaluma wa Jukwaa la Wahariri Jijini hapa.
Dilunga amesema hakuna kinachokwama ndani ya Benki hiyo kwani hata inapotajwa kuwa muda wa kazi umekwisha, huduma zinaendelea kutolewa kupitia NMB Wakala ambao wamesambaa nchi nzima .
Alisema matawi ya Benki yanakuwa wazi kila siku ya kazi kuanzia saa 2.30 asubuhi na muda wa kufunga hutegemea muda wa kazi Serikalini huku Mawakala wakiendelea kutoa huduma.
Meneja huyo amesisitiza NMB kuendelea kufanya kazi karibu na vyombo vya habari kupitia Wahariri ili taarifa za huduma za Benki ziwafikie watu wengi.
“Tunazo huduma nyingi sana, mfano tuko katika mpango wa teleza kidigitali, akaunti za watoto kwa ajili ya shule, mikopo kwa vikundi na Wastaafu lakini huduma zote zitajulikana ikiwa waandishi mtatoa taarifa sahihi kwa Watanzania na kwa upande wetu tuko tayari kufanya kazi na vyombo vya habari,” amesema Dilunga.
Kuhusu akaunti za watoto wa shule amesema zimekuwa mkombozi kwani huwawezesha Wazazi kuweka kidogo kidogo na mwisho wake inawasaidia vijana wao kutokukwama katika masomo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) Deodutus Balile aliwataja NMB kwamba wamekuwa ni sehemu ya kunisaidia jamii moja kwa moja na kupitia taasisi zingine katika kichagiza Maendeleo ya nchi.
Hata hivyo Balile aliutaja mkutano huo kuwa NMB ni miongoni mwa waliowezesha hadi kufanikiwa kwake hivyo akawaomba waendelee kuwa msaada hata wakati mwingine.
Mhariri na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dk Dotto Kuhenga aliomba NMB kuangalia uwezekano wa kuanza kazi saa 2.00 asubuhi ili waweze kusaidia watu wenye uhitaji na kutaka kuwahi makazini.
Dk. Kuhenga amesema ndani ya NMB kuna huduma nzuri zinazoendana na maisha ya sasa hivyo kama itawapendeza waone namna bora ya kuongeza huo muda.