Home KITAIFA KIMBUNGA HIDAYA CHAZIDI KUSOGEA ENEO PWANI

KIMBUNGA HIDAYA CHAZIDI KUSOGEA ENEO PWANI

Google search engine

Na MWANDISHI WETU

-DAR ES SALAAM

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa ya mwenendo wa Kimbunga Hidaya kilichopo katika Bahari ya Hindi Mashariki mwa Pwani ya Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya TMA imeeleza kuwa Kimbunga Hidaya kimeendelea kuimarika na kusogea kuelekea maeneo ya Pwani ya nchi ambapo hadi kufika saa tisa usiku kufika Mei 3, 2024 kilikuwa umbali wa takriban kilomita 401 Mashariki mwa Pwani ya Mtwara.

Nguvu ya Kimbunga Hidaya imeendelea kuimarika na kuwa kubwa zaidi, ambapo hadi kufikia usiku huu kasi ya upepo katika kimbunga imeimarika na kufika Kilomita 110 kwa saa na inatarajiwa kuendelea kuimarika zaidi katika kipindi cha saa 24 zijazo.

Mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa baharini bado inaonesha uwezekano mkubwa wa Kimbunga Hidaya kuendelea kusogea karibu kabisa na Pwani ya Tanzania na kuendelea kuwepo hadi Mei 6, 2024.

Hata hivyo, kimbunga hicho kinatarajiwa kupungua nguvu baada ya Mei 6, 2024.

Hatua ya uwepo wa Kimbunga Hidaya karibu na Pwani ya Tanzania unatarajiwa kutawala na kuathiri mifumo ya hali ya hewa hapa nchini ikiwa ni pamoja na kusababisha vipindi vya mvua kubwa na upepo mkali katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Dar es Salaam, Tanga, Morogoro, visiwa vya Unguja na Pemba na maeneo ya jirani.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here